22.9 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Watu saba mbaroni kwa kupandisha bei ya sukari

Amina Omari,Tanga 

BODI ya Sukari, imewatia mbaroni wafanyabiashara saba mkoani Tanga kwa kujihusisha na kuuza sukari zaidi ya bei elekezi iliyotokewa na Serikali hivi karibuni.

Afisa Miliki Mwandamizi wa Bodi ya Sukari, Mhandisi Ali Mwinyimanga alisema Serikali haitavumilia wafanyabiashara yoyote ambaye anaongeza bei kwa lengo la kuwaumiza wananchi,wakati tayari nchi inasukari ya kutosha.

“Hili ongezeko la sukari, ni la kutengeneza tuu,tulichogundua wafanyabiashara wametumia janga la vorona kueleza sukari imeadimika jambo ambalo halina ukweli,”alisema.

Alisema kazi ya kuwatafuta wafanyabiashara walanguzi ,ni endelevu mpaka pale wafanyabiashara watakapoweza kuuza kwa bei elekezi iliyowekwa na serikali.

“Tunachotaka ni kuhakikisha kuanzia mkulima ,mzalishaji hadi mtu wa mwisho ambaye ni mlaji anapata haki yake bila ya kumnyonya kama kule inapozalishwa bei haijapanda iweze wewe muuzaji ndio upandishe bei,”alisema.

Alisema ukaguzi huo, ni endelevu mpaka pale bodi ya sukari itakapojiridhisha kuwa sukari inauzwa kwa mujibu wa maelekezo yaliyotolewa na serikali.

Ofisa Mwandamizi Uchunguzi wa Tume ya Ushindani (FCC), David Mawi alisema tume ilipata malalamiko ya walaji kuhusu kuadimika kwa bidhaa hiyo pamoja na bei kubwa.

Alisema tume, imeamua kufanya uchunguzi ili kujiridhisha  na  malalamiko hayo kama yana ukweli kiasi gani.

“Tunachunguza kujiridhisha kama uhaba huo sio wa kutengeneza na washindani wa soko au kupangwa na washindani katika soko,” alisema.

Alisema baada ya kupata taarifa za kutosha kuhusu kero hiyo, watazifanyia kazi na kujana majibu ambayo yataweza kuwa suluhisho kwa wananchi ambao ni walaji wa mwisho

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,429FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles