25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Watu kadhaa wameripotiwa kuuawa Ethiopia

Tigray, Ethiopia

Nchi ya Ethiopia imeripoti vifo vya watu kadhaa na wengine kujeruhiwa kufuatiwa shambulio la ndege za kijeshi katika mji wa Togoga Jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia.

Mashambulizi hayo yamekuwa yakiendelea kwa muda wa miezi 8 dhidi ya Serikali ya Ethiopia yakipigana na vikundi vya waasi katika jimbo hilo.

Mapigano yameongezeka katika kipindi cha wiki mbili zilizopita huku wapiganaji wa Tigray People’s Liberation Front wakiiteka miji na vijiji.

Madaktari katika hospitali kuu ya Tigray Mekelle wanasema kuwa wanawatibu makumi ya watu akiwemo mtoto mwenye umri wa miaka 2 aliyejeruhiwa katika shambulio la anga siku ya Jumanne.

Lakini wahudumu wa matibabu wanasema wamezuia kufikia eneo la shambulio ili kuwasaidi walioachwa nyuma.

Walioshuhudia shambulio hilo waliliambia moja ya shirika la Habari kuwa ndege za vikosi vya serikali ya Ethiopia zilipiga makombora yake kwenye soko moja lililopo kilomita 25 kutoka Mekelle.

Jeshi la Ethiopia hata hivyo limekanusha madai ya kuwa lenga raia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,226FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles