23.9 C
Dar es Salaam
Thursday, September 29, 2022

WATU 8,000 KUNUFAIKA NA TASAF LINDI

Hadija Omary, Lindi


Jumla ya watu 8,000 wanaoishi Halmashauri ya Lindi, walio kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini, wanatarajiwa kunufaika na utaratibu wa kutekeleza shughuli za kukuza uchumi unaotekelezwa katika awamu ya tatu ya TASAF.

Hayo yameelezwa na Ofisa Mafunzo wa TASAF, Catherine Kisanga wakati wa kufunga mafunzo ya siku 10 kwa wawezeshaji katika ngazi ya mamlaka ya eneo la utekelezaji kuhusu mafunzo ya stadi za maisha.

Kisanga amesema wawezeshaji hao ambao wamepatiwa mafunzo wamejengewa uwezo kwa ajili ya kwenda kuwafundisha walengwa wa kaya masikini kuhusu stadi za maisha na ujasiriamali, kubuni wazo la biashara na kujua kukokotoa gharama za kuendesha biashara, pamoja na kuandaa mpango wa biashara ambao itawasaidia walengwa kuendeleza miradi yao.

“Katika programu hiyo, walengwa 80,000 watafikiwa kutoka Wilaya ya Lindi, ambapo kila mwezeshaji mmoja atafanya kazi na walengwa wapatao 60 kwa siku, mara mbili kwa siku yaani asubuhi na jioni,” amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, Samwel Gunza amewataka wawezeshaji hao kuhakikisha walengwa wanapata faida wanapofanya shughuli zao za kuzalisha mali ili kupata manufaa na kukabiliana na athari za umasikini.

“Wawezeshaji kutoka katika ngazi ya kata na vijiji wanategemewa kuwapatia walengwa utaalamu unaotakiwa katika shughuli zao za uzalishaji mali na pia kuwafuatilia na kuwapa msaada wa kitaalamu ili kuboresha shughuli zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,298FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles