27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WATU 75,000 WADAIWA KUISHI  NA VVU NJOMBE

Na Elizabeth Kilindi,Njombe

ZAIDI ya watu 75,000 mkoani Njombe, wanadaiwa kuishi na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi (VVU), kati yao 48,000 ndiyo waliojiunga kupata huduma za tiba na matunzo.

Lakini  wengi wao, wakiwa ni  wanawake, huku wanaume  27,00 hawajui hali zao.

Akizungumza juzi  wakati wa uzinduzi wa kampeni ya furaha yangu iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Bakita, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka alisema wanaume ambao hawajui hali zao za maambukizi wako katika hatari ya kuambikiza  watu wengine.

Alisema kupima na kuanza tiba matunzo mapema husaidia kuboresha hali ya afya na kupunguza uwezo wa kuambukiza wasio na maambukizi.

Alisema mkoa kwa kushirikiana na wadau unatoa huduma za VVU na Ukimwi katika vituo 237, vinatoa huduma ya mama na mtoto na vituo 62 vikiwa vinatoa huduma tiba na matunzo.

“Vituo hivi havitoshi, kuna wengine wanasafiri umbali mrefu kufuata huduma hii, nitumie nafasi hii kuagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuongeza vituo ikiwezekana kila kata mpango huu ukamilike haraka”alisema Ole Sendeka.

Alisema hadi mwishoni mwa Machi, mwaka huu,wanaume 16,734 pekee walikua wanatumia dawa za kupunguza makali ya VVU,wakati wanawake walikuwa 31,266.

“Wanaume tunajiita majasili hebu kwenye hili tuonyeshe ujasili wetu tulapime ili tujue hali zetu”alisema Ole Sendeka.

Kampeni ya Furah Yangu,Pima,Jitambue,Ishi, inahamasisha mkakati mpya wa Serikali wa upimaji wa VVU na kuanza kutumia ARV mapema.

Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe,Dk. Manyanza Mponeja alisema wanaume ambao kiwango chao cha upimaji kiko chini kwa asilimi 45.3, ukilinganisha na wanawake ambao ni asilimia 55.9.

“Kuna umuhimu sasa wa kuwahamasisha wanaume kupima na magonjwa mengine na ninawaomba wanawake waunge mkono kwa kuwa tayari mmeonyesha mfano mzuri wa kujali afya zao”alisema Mponeja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles