26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 29, 2023

Contact us: [email protected]

Watu 557 waokolewa biashara haramu ya binadamu

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

KATIBU wa Sekretarieti ya Taifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Seperatus Fella amesema kuwa watu 61 wamehukumiwa kwa kosa la kusafirisha binadamu na kesi 12 zikiendelea katika mahakama mbalimbali hapa nchini.

Hayo aliyasema jana Dar es Salaam katika kongamano la kujadili biashara haramu ya usafirishaji binadamu.

Alisema kuwa takwimu hizo ni za kuanzia mwaka 2016 hadi 2020, ambazo zinaongeza kuwa zaidi ya waathirika 557 wameokolewa baada ya kupata matatizo hayo na wanaendelea na shughuli zao nchini.

“Takwimu za 2016 hadi 2020 zinaonyesha kuwa watu waliohukumiwa ni 61, kesi 12 zinaendelea katika mahakama mbalimbali na wahanga wa biashara haramu ya binadamu hapa nchini ni 557,” alisema Fella.

Alisema kuwa changamoto kubwa ya kuendelea kuwepo kwa biashara haramu ya binadamu ni umasikini katika jamii kwani familia nyingi zinapokea fedha kidogo kwa kudanganywa na kutoa mtoto kwenda kufanya kazi mahali bila kujua kama ni kosa na pia biashara hiyo ufanywa kwa usiri mkubwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa sekretaireti hiyo, Adatus Magere alisema kuwa usafirishaji haramu wa bianadamu unashika nafasi ya tatu katika makosa makubwa ya kimataifa ikiongozwa na biashara haramu ya silaha na biashara ya dawa za kulevya.

“Watu wanaofanya biashara hii haramu inakuwa ni vigumu sana kuwapata mpaka vyombo vya sheria vinapowagundua, takwimu hazionekani katika uhalisia.

“Watu wengi wanachanganya tatizo la usafirishaji haramu wa binadamu na wahamiaji haramu kama ambao wamekuwa wakipitishwa hapa nchini kupelekwa Afrika Kusini, matatizo haya ni mawili tofauti, la kwanza ni kusafirishwa kwa hiari yao – ‘uhamiaji haramu’, na biashara haramu ya binadamu kwa anayesafirishwa anakuwa hajui malengo ya msafirishaji,” alisema Magere.

Kongamano hilo liliwashirikisha wadau mbalimbali kutoka taasisi za Serikali na binafsi na limefadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles