30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

WATU 40,000 WANAUGUA SARATANI

RAIS wa Taasisi ya Afya (THS), Dk. Omary Chillo (kulia)

 

Na PATRICIA KIMELEMETA –DAR ES SALAAM

RAIS wa Taasisi ya Afya (THS), Dk. Omary Chillo, amesema kila mwaka watu zaidi ya 40,000 wanaugua saratani.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Dk. Chillo alisema ongezeko la idadi ya wagonjwa hao hapa nchini ni kubwa na kuhatarisha maisha ya wananchi.

Alisema ongezeko hilo linatokana na sababu mbalimbali, ikiwamo ya matatizo ya maisha, vyakula na kutofanya mazoezi.

“Kuna ongezeko kubwa la wagonjwa wa kansa kila mwaka na katika miaka ya hivi karibuni wamefikia zaidi ya watu 40,000, jambo linaloonyesha wazi kuwa ugonjwa huo ni tishio na kwamba wananchi wanapaswa kupewa elimu ili waweze kubadili mtazamo wa maisha kwa namna moja au nyingine,” alisema.

Dk. Chillo alisema kati ya idadi hiyo, wagonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi na saratani ya matiti ni kubwa kuliko  saratani nyingine, hali inayoonyesha wazi kuwa tatizo hilo ni kubwa na wananchi wanahitaji kupewa elimu ili waweze kubadili mfumo wa maisha.

Pia alisema ugonjwa wa presha nao ni miongoni mwa magonjwa yanayoongezeka kwa kasi na takwimu za mwaka 2012 zimeonyesha ugonjwa huo umeongezeka hadi kufikia asilimia 26 na ugonjwa wa kisukari pia umefikia asilimia tisa.

Alisema magonjwa hayo kwa ujumla katika kipindi cha miaka iliyopita yalikuwa yanawapata watu wazima kuanzia umri wa miaka 55 na kuendelea, lakini sasa hivi yameshuka hadi kufikia miaka 35 na watoto wadogo, jambo linaloonyesha wazi kuwa kuna haja ya kuangalia chanzo cha tatizo na kutoa elimu kwa wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles