23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

WATU  21 KORTINI KWA KUUZA DAWA   BANDIA

Na JUDITH NYANGE


MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Ziwa imewafikisha mahakamani watu 21 kutoka katika mikoa ya kanda hiyo kwa miezi sita,  kwa tuhuma za kuuza dawa bandia na zile za serikali ya Tanzania.  

Watu hao walikamatwa na kufunguliwa mashitaka kutokana na  ukaguzi maalumu na  uhakiki uliofanywa na TFDA Kanda ya Ziwa kwa kuhusisha wakaguzi wa mamlaka hiyo   na  taasisi nyingine za udhibiti.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi na Meneja wa TFDA  Kanda ya Ziwa, Moses Mbambe,   kesi hizo zimefunguliwa katika mahakama za wilaya za Bariadi, Mugumu, Serengeti, Bukombe, Kahama, Tarime, Chato, Musoma na Maswa katika mikoa ya Geita, Shinyanga, Mara na Simiyu.

Mbambe alisema tayari kesi moja iliyofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma imeshatolewa uamuzi ambako ilimkuta na hatia Fatuma Daudi na kumhukumu kulipa faini ya Sh milioni moja  au kutumikia kifungo cha miezi 18 jela  endepo  atashindwa kulipa faini hiyo.

Mbambe alisema  kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Fatuma Daudi alikutwa akiuza dawa bandia na ambazo hazina usajili wa TFDA katika duka la dawa la  Wangwe lililopo mjini Musoma kinyume kifungu 76 (1) na (2) pamoja na kifungu 22 (1) (a) na 3 cha sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi namba moja ya mwaka 2003.

 “Anayetengeneza dawa bandia anasukumwa na nia ovu ya kujipatia fedha bila  kufuata taratibu huku akiwaumiza au kuondoa uhai wa watu wengine,  muuzaji au mtengenezaji wa dawa hizo anafanya hivyo kwa makusudi akijua kitendo hicho kinaweza kusababisha kifo kwa mgonjwa ambaye anatumia dawa ambayo haiwezi kumsaidia.

“Vitendo vya namna hii ni uuaji na havipaswi kuvumilika na  TFDA itaendelea kufanya ukaguzi za mara kwa mara katika soko   kubaini wote wanaojihusisha na biashara ya dawa bandia na ambazo hazina usajili kwa kuwa zinahatarisha uhai wa watu, chakula, vipodozi na vifaa tiba na kuziondoa   kulinda afya ya jamii,” alisema Mbambe.

Kuhusu dawa ambazo ni mali ya serikali ya Tanzania, Mbambe alisema TFDA imekuwa  ikizikuta dawa hizo zikiuzwa katika maduka ya watu binafsi kitendo ambacho ni kunyume na sheria.

“Sheria Kuu ya kanuni za adhabu (penal code) kifungu 312 A (2) kinatamka bayana kuwa ni kosa mtu yeyote kuhamisha au kumiliki au kuweka ndani ya jengo lolote au mahali popote, iwe pa wazi au pamefungwa mali za serikali ikiwamo dawa .

“Atakayekutwa navyo anaweza kutuhumiwa kuwa ameviiba au amevipata isivyokuwa kihalali na akishindwa kutoa maelezo ya kuiridhisha mahakama kuhusu namna gani alivyozipata, atakuwa anatenda kosa,” alisema Mbambe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles