24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

WATU 15,000 BADO WANAHITAJI KUOKOLEWA MSUMBIJI

Na Mwandishi Wetu

Watu wapatao 15,000 bado wanahitaji kuokolewa kutoka maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko baada ya kimbunga Idai kupiga eneo la kati la Msumbiji wiki iliyopita, Waziri wa Ardhi na Mazingira Celso Correia amesema

Waziri alisema wametambua kuwa watu 15,000 bado wanahitaji kuokolewa, watu hao wako katika hali mbaya. Bado wako hai, wanawasiliana nao, wanawapelekea chakula, lakini inawalazimu kuwaokoa na kuwaondoa katika maeneo hayo ya mafuriko.

Hadi Allhamisi asubuhi vifo 200 vimethibitishwa kutokea Msumbiji, zaidi ya 100 Zimbabwe na karibu 60 nchini Malawi. Mamia wamejeruhiwa na wengine wengi hawajulikani waliko. Zaidi ya watu milioni mbili na nusu wameathirika kutokana na upepo mkali na mvua zilizoletwa na kimbunga Idai katika eneo la Kusini mwa Afrika.

Wakati huo huo, Marekani yajiandaa kuanza shughuli za uokozi ambapo mpaka sasa Idara ya maendeleo ya kimataifa ya Marekani, USAID, imetangaza kuwa inasubiri kibali kutoka serikalini kuzindua mpango wa kupeleka timu ya kutoa misaada ya dharura ambapo itatumia ndege za kijeshi katika operesheni hiyo kufuatia janga la mafuriko yaliotokana na kimbunga Idai.

Tayari kuna ndege ya kijeshi ya Marekani Jijini Maputo ikisubiri amri ya Washington kuanza kusaidia kutoa huduma za dharura katika maeneo ambayo watu wamekwama kutokana na mafuriko hayo, ameleza afisa muandamizi wa USAID.

Nayo idara ya huduma za dharura ya Umoja wa Mataifa imetangaza kwamba imetenga dola za Marekani milioni 20 kutoka mfuko wa kukabiliana na dharura CERF ili kuhakikisha msaada unawasili katika maeneo yaliyoathirika zaidi.

Kwa upande wake Uingereza imetangaza msaada wa dola milioni 6 , huku Tanzania ikiwa imepeleka tani 238 za chakula na dawa kwa nchi tatu zilizoathirwa za Msumbiji, Malawi na Zimbabwe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles