26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Watu 150 wahakiki silaha Dar

DSC00265Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athumani, amesema zaidi ya watu 150 wamejitokeza kuhakiki silaha ikiwa ni mwendelezo wa kutii agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Akizungumza Dar es Salaam jana, alisema tangu kutangazwa kwa agizo hilo na Makonda Machi 18, mwaka huu wanaendelea kuhakiki silaha hizo huku Rais John Magufuli akiwa wa kwanza kufanya uhakiki.

“Baada ya Magufuli kufanya uhakiki wa silaha zake hivi karibuni, watu zaidi ya 150 wakiwemo viongozi mbalimbali waliopo serikalini, viongozi wastaafu, mabalozi wa nchi mbalimbali, wafanyabiashara na wabunge wamejitokeza kuhakiki silaha zao na wengine wameonyesha nia ya kufanya hivyo, hata hivyo tusingependa kutaja majina yao kwa sababu za kiusalama,” alisema Athumani.

Alisema lengo la kufanya uhakiki wa silaha hizo ni pamoja na kuboresha hali ya usalama, kuwajua watumiaji na kuwatambua tena wamiliki wa silaha hizo.

Alisema kwa sasa uhakiki huo utafanyika nchi nzima si kwa Dar es Salaam peke yake kama ilivyokuwa hapo awali.

Alisema wakazi wa Dar es Salaam wanaweza kuhakiki silaha zao katika vituo vya polisi vya Oysterbay, Temeke Chang’ombe, Ilala na Kituo cha Kati cha Dar es Salaam na wanatakiwa kwenda na  kitabu (firearm license book), picha ndogo nne za mhusika na anuani sahihi ya mahali anapoishi mhusika.

Pia aliwataka viongozi mbalimbali na wananchi wanaomiliki silaha kujitokeza kwa ajili ya kufanya uhakiki wa silaha zao huku akisisitiza kwa wakazi wa Dar es Salaam wanaweza kuonana na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro na mikoani wanaweza kuhakiki kwa makamanda wa mikoa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles