WATU 24 WAUWAWA KATIKA SHAMBULIO LA BOMU

0
430

Watu 24 wameuwawa kwa shambulizi la bomu kwenye mji mkuu wa Afghanistan Kabul.

Tukio hilo lilifanywa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga ambaye alijilipua katika eneo lenye washia wengi magharibi mwa mji.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Afghanistan, takriban watu 42 pia walijeruhiwa wakati wa mlipuko huo.

Lengo la shambulizi hilo halikutajwa mara moja na hakuna mtu aliyedai kuhusika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here