25.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

WATU 103 WAKAMATWA UGANDA KWA KUANDAMANA KUPINGA KUKAMATWA BOBI WINE

Jeshi la Polisi nchini Uganda limewakamata watu 103 katika maandamano yaliyozuka kupinga kukamatwa kwa mbunge wa upinzani Robert Kyagulanyi pamoja na wabunge wengine kadhaa nchini humo.

Pia imearifiwa kuwa mtu mmoja ameuawa katika ghasia hizo.

Katika maandamano hayo, waandamanaji wamechoma moto magurudumu ya magari, wamerusha mawe huku wakiweka vizuizi barabarani na kufunga baadhi ya barabara lakini vikosi vya usalama vya Uganda vilisambaratisha maandamano hayo kwenye mji mkuu Kampala.

Bobi Wine alikamatwa na kushtakiwa kwenye Mahakama ya kijeshi wiki iliyopita kufuatia madai kuwa alikuwa anamiliki silaha kinyume cha sheria.

Watu wengi wanayahusisha mashtaka hayo na mbinu za kisiasa dhidi ya viongozi wa upinzani nchini Uganda.

Ghasia inaongezeka mjini Kampala kufuatia kukamatwa kwa mbunge Bobi Wine. Ripoti zimeibuka kuwa aliteswa akiwa mikononi mwa wanajeshi. Rais Yoweri Museveni amekana madai kuwa Bobi Wine alijeruhiwa.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles