29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

WATU 10 WAFARIKI DUNIA KWA KUGONGWA NA GARI MAKUSUDI

TORONTO, CANADA


POLISI mjini hapa wamemtambua dereva aliyeua watu 10 na kujeruhi wengine 15 kwa gari lake wakati wakitembea kando mwa barabara katika muda wa saa za mchana.

Mkuu wa Jeshi la Polisi mjini hapa, Mark Saunders, alimtaja mshambuliaji kuwa ni Alek Minassian mwenye umri wa miaka 25, mkazi wa Kitongoji cha Richmond Hill.

Saunders alisema Minassian hakuwa mtu aliyekuwa anatambulika na polisi kwa kuhusika na vitendo vya aina yoyote vyenye kutia shaka.

Aidha taarifa kutoka kwenye mitandao ya jamii, zinasema kijana huyo ni mwanafunzi wa chuo kikuu.

Kwa mujibu wa Saunders, dalili zinaonyesha wazi mtu huyo alitenda kosa hilo kwa kudhamiria na alijaribu kukimbia, lakini polisi walifanikiwa kumkamata na kwa sasa anashikiliwa.

Alisema polisi wanachunguza kiini cha kufanyika kwa shambulio hilo na kwamba mtuhumiwa huyo angefikishwa mahakamani baadaye jana.

Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau, alisema shambulio hilo ni baya na la kijinga, na kwamba ni moja ya mashambulizi ya kutisha zaidi katika historia ya karibuni ya Canada.

Alisema raia wote wanapaswa kujisikia wako salama kutembea katika miji na miongoni mwa jamii.

Trudeau alisema hali hii inafuatiliwa kwa ukaribu na kwamba Canada itaendelea kufanya kazi na vyombo vya usalama nchini kote kuhakikisha usalama wa wananchi wake.

Tukio hilo limefanyika wakati ambao mawaziri wa mambo ya nje kutoka kundi la nchi saba zinazoongoza kiviwanda duniani (G7) wanakutana hapa kujadili masuala ya kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles