27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

WATOTO WENYE VICHWA VIKUBWA WAFANYIWA UPASUAJI

Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM


JUMLA ya watoto 30 wenye vichwa vikubwa wamefanyiwa upasuaji na Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI).

Upasuaji huo umefanikiwa baada ya jumuiya ya madhehebu ya Shia kuchangia gharama za matibabu na damu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Meneja Uhusiano na Ustawi wa Jamii wa MOI, Jumaa Almasi,  alisema katika upasuaji huo meza tatu zilitumika ambapo kila moja ilifanikiwa kuwahudumia watoto 10.

Alisema afya za watoto hao zinaendelea vizuri na bado wanaendelea na uchunguzi na matibabu zaidi.

“Tumefanikiwa kufanya upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa 30 baada ya kupata fedha za matibabu na damu kutoka jumuiya ya madhehebu ya Shia,” alisema Almasi .

 Alisema upasuaji huo umefanikiwa kutokana na kupokea msaada wa fedha na damu kutoka jumuiya hiyo.

“Tunawashukuru ndugu zetu wa madhehebu ya Shia kwa kuchangia gharama za matibabu na damu,”alisema Almasi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles