26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Watoto wataka wanaotupa watoto wakamatwe

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

WATOTO wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi jijini Dodoma, wameiomba Serikali kuwachukulia hatua wazazi ambao wamekuwa wakiwatupa watoto.

Kilio hicho kimetolewa jana jijini hapa na watoto wanaolelewa katika Kituo cha Rahmani Orphanage Center kilichopo Chang’ombe, jijini hapa wakati walipokuwa wakitoa shukrani baada ya kusaidiwa misaada ya chakula iliyotolewa na Jumuiya ya Waislamu ya Ahmadiyya, Kanda ya Kati.

Akizungumza kwa niaba watoto wenzake, mtoto Saluma Alfani, aliiomba Serikali kwa kupitia vyombo husika, kutowafumbia macho wazazi wanaowatupa watoto kwa kuwa kutupa mtoto ni kosa kisheria.

Alisema kwamba, kitendo hicho ni cha kikatili na kinatakiwa kukemewa kwa nguvu zote kwani kinaisababishia Serikali hasara ya kuwalea watoto hao.

“Watoto wengi wanaolelewa kwenye vituo, asilimia kubwa hawana wazazi baada ya kutelekezwa na kitendo hicho ni cha kikatili na pia Serikali na jamii imekuwa ikiingia gharama kubwa ya kuwahudumia watoto hao.

“Pamoja na taasisi nyingi kujitokeza kwenye utoaji wa misaada kama ilivyo kwa Jumuiya ya Ahmadiyya walivyotoa misaada yao kwetu, bado Serikali inalo jukumu la kuhakikisha suala la utupaji wa watoto linakomeshwa na wahusika wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria,” alisema mtoto Saluma.

Naye mwakilishi wa kituo hicho, Hamisi Ramadhan, alisema changamoto kubwa iliyopo kwenye vituo vya kulelea watoto ni ukosefu wa wazazi wenye watoto hao ambao kwa asilimia kubwa waliwatupa na wengine kuwakimbia kutokana na hali ngumu ya maisha.

Kwa upande wake, Sheikh wa jumuiya hiyo, Khawaja Muzafar, alisema misaada iliyotolewa kwa kituo hicho ni sehemu ya kuadhimisha siku ya jumuiya yao iliyoanzishwa Machi 23, mwaka 1889. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,631FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles