29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

Watoto wampa Klopp jeuri ya kutosajili

Jurgen KloppLIVERPOOL, ENGLAND

KOCHA wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp, amedai kwamba wachezaji wake wenye umri mdogo wanaonesha mabadiliko makubwa hivyo hakuna ulazima sana wa kusajili kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.

Timu hiyo juzi ilishuka dimbani kupambana na wapinzani wao, West Ham kwenye Kombe la FA na mchezo huo ulimalizika kwa kutoka sare ya bila kufungana.

Katika mchezo huo, Klopp alijaribu kuwapa nafasi wachezaji wake wenye umri mdogo na kuvutiwa na kiwango chake ambapo anaamini kuwa wakipewa nafasi wana uwezo mkubwa wa kubadilisha mchezo.

“Ligi imekuwa ngumu na inahitaji wachezaji kujituma zaidi kwa ajili ya timu, bado ninaamini nina kikosi bora ambacho kinaweza kuleta mabadiliko kwenye ligi.

“Tumetoka bila ushindi kwenye mchezo wa FA dhidi ya West Ham, hainipi sababu ya kuhangaika kutafuta wachezaji wa kusajili waliopo wanatosha japokuwa kulikuwa na uwezekano wa kuongeza wachezaji,” alisema Klopp.

Kesho Liverpool itashuka dimbani kupambana na vinara wa Ligi Kuu nchini England, Leicester City katika michuano ya ligi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles