22.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Watoto waliopotea Mbeya wakabidhiwa kwa wazazi wao

MURUGWA THOMAS -TABORA

SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imewakabidhi kwa wazazi wao watoto wawili waliopotea Mkoani Mbeya baada ya kupatikana wakiwa na mama mmoja akiwa hospitali ya wilaya ya Nzega ambaye jina lake limehifadhiwa kwa taratibu za usalama.

Disemba 28 mwaka uliopita watoto Faisal Mashaka (5) na Anna Mashaka mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi sita walipotea nyumbani kwao mkoani Mbeya wakati wakicheza jirani na nyumba yao.

Taarifa za kupotea kwa watoto hao zilifikishwa Polisi na wazazi wao pamoja na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii ambapo mmoja alipatikana mjini Nzega na mwingine katika Manispaa ya Tabora.

Watoto hao walikabidhiwa kwa wazazi wao na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri  mbele ya Maaskofu Dk. Vallentino Mokiwa na Dk. Elias Chakupewa wa Kanisa la Anglikani Dayosisi ya Magharibi.

Akikabidhi watoto hao, Mkuu wa Mkoa wa Tabora ametoa onyo kwa wale wote wanaohusika na vitendo vya aina hiyo na kwamba Serikali itahakikisha inawachulia hatua kali za kisheria.

Mbali ya hilo, Mkuu huyo wa Mkoa ametoa tahadhali kwa wazazi kuwa karibu na watoto wao badala ya kuwategema wasaidizi wa kazi ndio watumike kuwalea muda mwingi ili kujiepusha na majnga kama haya.

Mwanri pia amewashukuru wananchi kwa ushirikiano wao waliouonyesha na kusaidia kupatikana kwa watoto hao wakiwa na afya njema.

Nao wazazi wa watoto hao wametoa shukrani kwa wananchi wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine kufanikisha kupatikana kwa watoto wao wakiwa salama.

Mashaka Juma baba mzazi wa watoto hao ambaye ni Ofisa Afya wa Mkoa wa Mbeya alisema kitendo cha kupatikana kwa watoto wake wakiwa hai hakukitarajia kutokana na mazingira ya kutatanisha walivyopotea wakiwa mikononi mwa dada wa kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,526FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles