22.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Watoto wafungwa kwa kumshambulia mama yao

Na Tausi Ally, Mtanzania Digital

MTU na Dada yake wamehukumiwa kwenda jela miaka minne kwa kumtukana na kumpiga mama yao Maria Vazi.

Washtakiwa hao, Zulfikar Safraz na Nurin Safraz wametiwa hatiani leo Novemba 15, saa sita mchana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Rehema Liana.

Hakimu Liana amesema Mahakama imekubali rufani iliyokatwa na mama yao akipinga watoto hao kuachiwa huru na Mahakama ya Mwanzo Kariakoo.

Amesema hoja ya iliyowaachia huru kwamba hakukuwa na PF 3 haikuwepo kwa pande zote mbili, aliibua hakimu na kuijibu hivyo haina mashiko.

Mashahidi wote watatu walithibitisha kwamba watoto walimpiga na kumtukana mama yao hivyo mahakama inawatia hatiani mwa makosa yao.

Hakimu Liana amesema amezingatia maombi ya watoto hao kuwa wanaomba Mahakama iwapunguzie adhabu kwa sababu wanaumwa ugonjwa wa Pumu na vidonda vya tumbo na kwamba hawatarudia tena makosa ya namna hiyo kwa Mama yao.

“Ili iwe fundisha na onyo kwa wengine wenye tabia kama hizi kila mmoja ata kwenda jela miaka minne,” amesema Hakimu Liana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles