27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Watoto wafanyiwa upasuaji wakiwa tumboni mwa mama

IMEZOELEKA kwa mtu kufanyiwa upasuaji kwa ajili ya kuokoa uhai wake au kurekebisha kiungo au viungo vyenye matatizo.

Mara nyingi jambo hili hufanyika kwa mtu ambaye ameshazaliwa na si yule aliyepo tumboni kwa mama yake.

Kwa mara ya kwanza madaktari nchini Uingereza wamewafanyia upasuaji watoto wawili ambao bado hawajazaliwa.

Upasuaji huo uliofanyika wiki chache kabla ya kuzaliwa kwao, ulifanywa na kundi la madaktari 30 wa chuo kimoja jijini London.

Watoto hao walikuwa na tatizo linaloitwa spinal bifida, ambapo uti wa mgongo hushindwa kukua vile inavyotakiwa.

Mara nyingi hali hiyo hutibiwa baada ya mtoto kuzaliwa, lakini ikiwa itatibiwa mapema hali ya afya ya mtoto huwa bora zaidi.

Wakati wa upasuaji huo uliochukua muda wa dakika 90, madaktari walipasua tumbo la mama kisha wakashona pamoja sehemu ya uti wa mgongo wa mtoto iliyokuwa imeachana.

Upasuaji huo ni hatari na unaweza kusababisha mama apatwe na uchungu wa kujifungua mapema kabla ya muda wake kufika.

Wajawazito ambo watoto wao waligundulika kuwa na tatizo hilo nchini Uingereza walihitaji kwenda nchini Marekani, Ubelgiji au Uswizi kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.

Kwa mujibu wa Shirika la Charity Shine, zaidi ya watoto 200 huzaliwa na hali hiyo ya spina bifida kila mwaka.

Hali hiyo hutokea wakati kitu kinachoitwa neural tube – awamu ya kwanza ya kukua kwa ubongo na uti wa mgongo hukua kwa njia isiyostahili na kusababisha kuwapo nafasi kwenye uti wa mgongo.

Upasuaji unaweza kutumia kuziba nafasi hiyo kwenye uti wa mgongo, lakini mara nyingi matatizo yatakuwa tayari yametokea na miguu kupooza.

Kinachosababisha hali hiyo hakijulikani, ambayo hutokea wakati ambao mtoto huendelea kuumbwa tumboni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles