21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

WATOTO WAELIMISHWE UBAYA WA RUSHWA KUANZIA SHULENI

Na LEONARD MANG’OHA


WAKATI wa mkutano wa 29 wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia mwaka jana, walikubaliana kwa kauli moja kwamba Julai 11 kuwa siku ya mapambano dhidi ya rushwa barani humo.

Waliamua kuwa mwaka 2018 utakuwa wa mapambano dhidi ya rushwa chini ya kauli mbiu isemayo; ‘Ushindi katika vita dhidi ya rushwa: njia ya kuleta mabadiliko chanya barani Afrika.

Kwa maneno mengine ni kwamba siku hiyo ilianza kuadhimishwa rasmi jana ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanyika.

Lengo la kuanzishwa kwa siku hii ni kupata fursa ya kutafakari athari za rushwa kwa maendeleo na ustawi wa bara zima la Afrika ikiwamo Tanzania.

Maadhimisho haya yanaanza wakati Tanzania tayari ikiwa katika mapambano makali ya kukabiliana na rushwa na ufisadi katika sekta ya umma na binafsi pamoja na mfumo wa siasa ambao unatajwa kutawaliwa na rushwa hususan wakati wa chaguzi mbalimbali.

Ni wazi kuwa rushwa katika mataifa mengi imehalalishwa kwa namna moja au nyingine kutokana na maeneo mengi ikiwamo mahakama na idara zingine kudaiwa kutawaliwa na rushwa kiasi cha kuwakosesha watu haki wanazostahili kwa sababu tu hawakupenda ama hawakuweza kutoa rushwa.

Kwa kuwa viongozi wakuu barani Afrika wameliona hili kama kikwazo cha ustawi na maendeleo kwa bara letu, ni wazi kuwa watatoa msukumo wa kina kuhakikisha wanakabiliana na adui huyu wa haki.

Tangu kuingia madarakani kwa Rais Dk. John Magufuli, amekuwa akijipambanua kuwa ni mpinga rushwa katika mifumo yote ya nchi ambapo ni katika kipindi hiki baadhi ya vigogo wa kisiasa na wasio wa kisiasa wakipandishwa kizimbani kwa tuhuma za rushwa.

Kutokana na nia yake hiyo, aliyoionesha ni vema ikaungwa mkono na kila mchukia rushwa ili kuleta usawa katika jamii.

Lakini tutambue kuwa rushwa hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine, hivyo ni vema kuhakikisha kunakuwapo mfumo wa kudhibiti vitendo vya hivi kwa kutoa elimu kwa watoto tangu wakiwa wadogo kuanzia shuleni hata katika nyumba za ibada ili kuwafanya watambue rushwa si haki ya mtu.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles