27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

‘Watoto vichwa vikubwa wapewe bima ya afya’

big-headed1JOHANES RESPICHIUS-DAR ES SALAAM

SERIKALI imeombwa kuwakatia bima za afya watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na migongo wazi wenye umri chini ya miaka mitano ili kurahisisha upatikanaji wa matibabu kwa watoto hao.

Hayo yalibainika jana jijini Dar es Salaam katika mkutano wa mwaka wa Chama cha Wazazi wa Watoto Wenye Vichwa Vikubwa na Migongo Wazi (ASBAHT), ambao pia uliwahusisha madaktari bingwa wa magonjwa hayo.

Akizungumza katika mkutano huo, Daktari bingwa wa upasuaji wa watoto, Dk. Catheren Mlelwa, alisema ni vyema Serikali ikaweka utaratibu wa kumpatia bima ya afya pale tu anapozaliwa ambayo ataitumia mpaka atakapo timiza miaka mitano.

“Kwa kuwa Serikali huwa inasema kuwa inatoa huduma ya afya kwa mtoto wa chini ya miaka mitano bure ni vyema ikaweka utaratibu wa kutoa bima za afya kupitia Mfuko wa Bima wa Taifa NHIF kwa watoto hawa pale tu wanapozaliwa ili kuondoa changamoto ya matibabu,” alisema Dk. Catheren.

Kwa upande wake Makamu wa rais wa Taasisi ya Friends of Chilgren within Cancer, Walter Miya, aliilalamikia NHIF, Mkoa wa Mwanza kwa kumkatalia kukata bima kwa watoto wenye tatizo la vichwa vikubwa na migongo wazi.

“Niliwapeleka watoto wangu ili wakatiwe bima ya afya katika mfuko wa bima wa NHIF mkoani Mwanza cha kusikitisha baada ya yule mtoa huduma kuona picha kwamba wana tatizo la vichwa vikubwa alikataa kunikatia ile bima kwa kusema kuwa hawapaswi kukatiwa bima,” alisema Walter.

Naye Mkurugenzi wa tiba wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dk. Samuel Swai, alisema kuwa hakuna sababu ya mashirika ya bima kukataa kuwakatia bima za afya watoto wenye tatizo la vichwa na migongo wazi kwa kuhofia gharama kuwa nyingi.

“Gharama za kumtibu mtoto mwenye tatizo hili ni za kawaida hivyo sioni kama kuna sababu yoyote kubwa ambayo inaweza kuifanya mifuko ya bima hasa kwa shirika la Serikali kukataa kumtakia bima mtoto mwenye kichwa kikubwa na mgongo wazi,” alisema Dk. Swai.

Aidha alendelea kuwata wazazi wenye watoto wa matatizo hayo kutowaficha na badala yake wawafikishe mapema Hospitalini ili mtoto aweze kufanyiwa vipimo na kupatiwa matibabu kwani ujongwa huo unatibika kama ukiwaiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles