23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

Watoto milioni 12 kupata chanjo ya surua, polio

AVELINE KITOMARY – DAR ES SALAAM

MENEJA Mpango wa Taifa wa Chanjo, Dk. Dafrossa Lyimo, amesema Sh bilioni 11 zitatumia kwa kampeni ya surua ya rubella na polio kwa watoto milioni 12 wenye umri wa chini ya miaka mitano.

Kampeni hiyo ambayo inatarajia kuanza Septemba 26 hadi 30, itahusisha utoaji elimu kwa jamii na utoaji bure wa chanjo kwa maeneo yote nchini.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na MTANZANIA, Dk. Lyimo alisema lengo la kampeni hiyo ni kupunguza au kutokomeza kabisa magonjwa hayo.

 “Tunatarajia kufanya kampeni ya surua rubella, na kampeni hizi zilianza mwaka 2014 kutokana na ugonjwa huu kuathiri sana watoto, mfano inasababisha mtoto kupata homa kali, ubongo kuathirika, macho, mwli kuota vipele, kuharisha na kupata nimonia.

 “Hivyo lengo letu la kutoa chanjo ni kuendelea kupunguza au ikiwezekana kutokomeza kabisa ugonjwa wa surua ya rubella na polio.

“Mwaka 2014 tulianza chanjo ya rubella ambayo inasababisha mtoto kuathirika moyo, figo, maini, uti wa mgongo, hii inapotokea ama amepata, madhara yake yanaenda kwa mtoto,” alieleza Dk. Lyimo.

Alisema changamoto zilizopo sasa ni uelewa mdogo wa jamii kuhusu jinsi ya utoaji wa chanjo hizo hali inayosababisha watoto wengine kukosa chanjo zote.

 “Tatizo linakuja pale ambapo watoto hawamalizi chanjo kwa sababu kuna chanjo mbili, wengine wakipata dozi ya kwanza ambayo inatolewa kwa mtoto wa miezi tisa,  hawarudi kupata ya pili ambayo inatolewa baada ya mtoto kutimiza miezi 18.

“Changamoto nyingine ni uhamasishaji kwa ngazi za chini ni mdogo, mfano viongozi wa vijiji, mitaa, kata wanatakiwa kuhamasisha watu, pia elimu ya chanjo bado haijawafikia watu wengine,” alisema Dk. Lyimo.

Alitoa ushauri kwa jamii kuzingatia chanjo kwa watoto wao kwani zinamkinga mtoto dhidi ya magojwa 13.

 “Wazazi wanatakiwa wahakikishe wanashiriki katika zoezi la utoaji wa chanjo kwa watoto wao kwani chanjo zinazotolewa zinamkinga mtoto na magonjwa mengi tu kama polio, kifaduro, surua, pepopunda na mengineyo,” alisema.

HALI ILIVYO SASA

Dk. Lyimo alisema kwa sasa ugonjwa wa surua ya rubella umepungua kwa asilimia 95, huku Tanzania ikiwa ni nchi ya tatu barani Afrika kwa kudhibiti magonjwa hayo kwa watoto.

Alisema kwa dozi ya kwanza ya surua ya rubella asilima 99 ya watoto wa miezi tisa wanapata huku dozi ya pili ya miezi 18 ni asilimia 84 ya watoto wanapata.

 “Kuna watoto wengine miili yao haipati chanjo haraka kutokana na kinga za miili yao, hivyo asilimia 25 pamoja na kuchanjwa wanapata surua kutokana na hali ya miili yao na kuna wale ambao hawajachanjwa kabisa, hao wanaweza wakawa wachache sana,” alisema Dk. Lyimo.

Alisema kuwa mpango wa kidunia ni kuhakilisha mwaka 2020 ugonjwa huo uwe umeshatokomezwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles