WATOTO MILIONI 1.1 VENEZUELA WATAHITAJI MSAADA MWAKA 2019

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) limesema kufuatia mzozo wa Venezuela takriban watoto milioni 1.1 ikiwemo waliolazimika kukimbia kutoka Venezuela, wale ambao wanarejea nyumbani na wale walioko katika jamii zinazowahifadhi au safarini watahitaji ulinzi na huduma za msingi katika ukanda wa Amerika ya Kusini na Carribea mwaka huu wa 2019.

Hili ni ongezeko kutoka kwa watoto 500,000 walio na mahitaji kwa sasa ambapo UNICEF imetoa wito kwa serikali katika ukanda huo kuhakikisha haki za watoto hao ikiwemo wahamiaji na wakimbizi zinalindwa na kuhakikisha kwamba wanapata huduma muhimu.

Kwa mujibu wa wadau wa misaaada ya kibinadamu, watu milioni 4.9 katika ukanda huo wakiwemo kutoka Brazil, Colombia, Ecuador, Guyana, Panama, Peru na Trinidad na Tobago wanahitaji msaada kwani hali iliyopo Venezuela inawafanya watu wengi kuhama, kwa mfano  msichana Alegny msichana mwenye umri wa miaka 12

Cristina Perceval ambaye ni Mkurugenzi wa UNICEF ukanda wa Amerika Kusini na Carribea anasema UNICEF inafanya kazi na wadau kutoa huduma za maji safi, masuala ya kujisafi, elimu, ulinzi na huduma za afya.

UNICEF imeeleza kusikitishwa na ripoti za chuki dhidi ya wageni, ubaguzi na ukatili unaotekelezwa dhidi ya watoto waVenezuela na familia zao katika jamii zinazowahifadhi.

UNICEF imetoa ombi la dola milioni 69.5 kwa ajili ya msaada kwa watoto waliofukuzwa kutoka Venezuela na wanaoishi katika jamii zinazowahifadhi na walio safarini katika sehemu mbalimbali katika ukanda wa Amerika ya Kusini na Carribea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here