31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

WATOTO HUTAMANI KUFANYA KAZI KWA KUWAONA WATU WANAOWAFAHAMU

Na MWANDISHI WETU


UTAFITI wa Kimataifa umebaini kuwa watoto katika mataifa yanayoendelea mara nyingi huwa na shauku ya kufikia malengo ya juu kuliko wavulana katika mataifa ya Uingereza.

Wakati wavulana nchini Uingereza wakiwa na malengo ya kuwa wachezaji wa mpira wa miguu au watu maarufu katika mtandao wa YouTube, wenzao nchini Uganda na Zambia wanataka kuwa madaktari na walimu.

Matokeo ya utafiti huu yaliwasilishwa kwa viongozi wakuu wa kibiashara duniani mjini Davos.

Watafiti waliwaambia watoto wa shule ya msingi wenye umri kati ya miaka 11 katika mataifa 20 kuchora picha za kazi wanazotaka kufanya watakapokuwa watu wazima.

Baada ya zoezi hilo, walibaini kwamba kasumba ya kijinsia kwa kiwango kikubwa huanza kujikita tangu utotoni.

Nchini Uingereza, wasichana wachache walipendelea kuwa wahandisi au wanasayansi, lakini kazi kama uuguzi, uchezaji ngoma na ususi zilikuwa ni miongoni mwa kazi 10 zilizochaguliwa na wasichana. Wavulana nao walichagua zaidi urubani na umakenika.

Wasichana walijikita zaidi katika mafanikio ya kitaaluma, ambayo yangeambatana na kazi kama ualimu, matibabu ya mifugo na udaktari.

Kwa mfano, wavulana walionekana kuvutiwa zaidi na tamaduni maarufu zikishabihiana na kazi kama uanamichezo, kazi katika mitandao ya kijamii au upolisi.

Watafiti walibaini na kuelekeza kwamba ni vyema kutambulisha kazi na mifumo mbalimbali ya majukumu kwa watoto wakiwa katika umri mdogo.

Wasichana katika shule ambazo zinaonekana kuwa na hali duni, wengi wao walitaka kuwa wauza duka au wataalamu wa urembo huku wavulana katika shule bora wakitaka kuwa mameneja na wanasheria.

Nje ya Uingereza, michoro ilionyesha kiu na shauku ya hali ya juu licha ya mazingira magumu katika mataifa hayo.

Uganda na Ufilipino wasichana wengi walitaka kuwa walimu, wakati nchini Pakistan, Bangladesh, Colombia na Indonesia walitaka kuwa madaktari.

Nchini China, kazi maarufu kwa wavulana ni uanasayansi. Lakini Uingereza na kwingineko kimataifa kulikuwa na tofauti kubwa kati ya mahitaji ya soko la ajira na shauku walizo kuwa nazo vijana.

Watafiti hawa wanasema kutokuwa na mpangilio bado kumeendelea kuwa kikwazo kwa wanafunzi hawa na kutoendelea kujua ni maarifa yapi wanatakiwa kuwa nayo kwa ajili ya kazi wanazozipenda.

Msimamizi wa utafiti wa kielimu, Andreas Schleicher anasema shauku ya watoto hawa inachochewa na watu wanaowajua au kuwafahamu.

Anne Lyons, Rais wa Chama cha Taifa cha walimu wakuu nchini Uingereza, anasema utafiti huu unaonyesha ilivyo ngumu kwa watoto hawa kuivunja mitazamo waliyojengewa na familia zao.

Nchini Uingereza kazi maarufu kwa wasichana ni pamoja na ualimu, maafisa wa matibabu ya mifugo, uanamichezo, udaktari, usanii, uanamuziki, ususi, uanasayansi, unenguaji na uuguzi.

Kwa upande wa wavulana, kazi wanazopendelea ni uanamichezo, utaalamu mitandaoni, polisi, uanajeshi, uanasayansi, uhandisi, udaktari, ualimu, maafisa wa matibabu ya mifugo na umakenika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles