26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Watoto 700 wafanyiwa upasuaji wa moyo JKCI

Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi
Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

WATOTO 728 waliokuwa wamezaliwa na magonjwa ya moyo wamefanyiwa upasuaji katika Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Upasuaji huo umefanyika tangu mwishoni mwa mwaka jana hadi kufikia Septemba, mwaka huu.

Mkuu wa Kitengo cha Uchunguzi wa taasisi hiyo, Pedro Pallangyo alisema hayo jana wakati taasisi hiyo ilipopatiwa msaada wa zaidi ya Sh milioni 300.

Alisema fedha hizo zimetolewa na benki ya I & M, taasisi isiyo ya kiserikali ya Bap Charity na   ‘Youth Welfare Trust’ na itatumika kwa upasuaji wa watoto zaidi ya 20.

“Katika kipindi cha mwaka jana, watoto 234 walifanyiwa upasuaji kwa kutumia mtambo maalumu (cath lab) ambako tuliwafanyia upasuaji bila ya kufungua kifua  na wengine 204 walifanyiwa kwa kufungua kifua.

“Mwaka huu, Januari hadi Septemba, katika cath lab tumewafanyia upasuaji watoto 494 sawa na asilimia 200 na ule wa kufungua kifua watoto 234 sawa na asilimia 116 tukilinganisha na mwaka jana,” alisema.

Naye Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi alizishukuru taasisi hizo kwa msaada huo na kuwaomba wadau wengine wajitokeze kufadhili matibabu ya watoto waliozaliwa na magonjwa hayo.

“Leo wametupatia kwa sababu wanaona juhudi ambazo tumezionyesha kufanikisha matibabu ya watoto kwa kiwango cha asilimia 98, lakini bado watoto wanaendelea kuzaliwa na matatizo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,663FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles