28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Watoto 65 wabakwa, kulawitiwa Kinondoni

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Watoto 65 wamebakwa na kulawitiwa katika Wilaya ya Kinondoni kwa kipindi cha Julai hadi Agosti mwaka huu.

Takwimu hizo zimetolewa Novemba 8,2024 na Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Kinondoni, Christian Nyakizee, wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha Julai hadi Agosti mwaka huu.

Amesema watoto 36 walibakwa na kulawitiwa mwezi Julai na watoto 29 mwezi Agosti wastani wa mtoto mmoja kila siku.

“Tunaomba wananchi wachukue hatua dhidi ya vitendo vya rushwa vinavyochangia kutendeka kwa makosa ya ukatili wa kijinsia na rushwa ya ngono ambavyo vinamalizwa kwa makubaliano.

“Tutaendelea kupokea malalamiko yote yanayohusu rushwa na kuyafanyia kazi kwa haraka ili kudhibiti vitendo vya rushwa wakati wote,” amesema Nyakizee.

Amesema pia wamechukua jitihada za kutoa mafunzo kwa maafisa ustawi wa jamii 25 na askari polisi 37 wa Dawati la Jinsia na Watoto ili kutatua kero ya ukatili wa kingono kwa watoto na jamii unaochangiwa na vitendo vya rushwa.

Aidha amesema katika kipindi hicho wamepokea malalamiko 104 na kati ya hayo 72 yalihusu rushwa na yasiyohusu rushwa ni 32.

Kuhusu miradi ya maendeleo amesema wamekagua miradi sita yenye thamani ya Sh bilioni 15.9 ambapo wamebaini mapungufu machache na wahusika wameshauriwa kurekebisha.

Kaimu Mkuu huyo wa Takukuru Kinondoni amesema kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wanaendelea kuelimisha wananchi wajue madhara ya rushwa na wahamasike kushirikiana na taasisi hiyo kuitokomeza.

Taasisi hiyo imetoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano na kuwasihi wapatapo taarifa za rushwa watoe taarifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles