25.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

WATOTO 510 WAKOSA FEDHA MATIBABU YA MOYO

 

 

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

WATOTO 510 waliozaliwa na magonjwa ya moyo, bado wapo kwenye foleni ya kusubiri matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kutokana na wazazi wao kukosa fedha.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto, Dk. Naiz Majani, wakati wa ziara ya Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, aliyefika hospitalini hapo kufuatilia matibabu ya mtoto Dorine Sestenes (3) ambaye taasisi yake ya Tulia Trust imefadhili matibabu yake.

Dk. Majani alisema mtoto huyo amezaliwa na tatizo la tundu kwenye moyo lililopo katikati ya vyumba vya juu na chini, ambavyo husababisha damu chafu kuchanganyika na damu safi.

“Watoto hao wanasubiri matibabu, tunashindwa kuwafanyia upasuaji, wazazi wengi wana changamoto ya kifedha,” alisema Dk. Majani.

Kwa upande wake, Dk. Tulia, aliwataka wananchi na viongozi kujitokeza kusaidia kuwezesha matibabu ya watoto hao.

“Tumeelezwa kuna zaidi ya watoto 500 ambao wanasubiri upasuaji, wengi wazazi wao wana maisha duni.

“Hivyo ni vizuri sisi ambao Mungu ametujalia afya njema kuwasaidia wenzetu, angalau kila mmoja amsaidie mtoto mmoja, naamini tutafanikisha matibabu ya watoto hawa,” alisema.

Pia alisema Taasisi ya Tulia Trust itaendelea kufuatilia kwa ukaribu matibabu ya mtoto Dorine.

“Nimemjulia hali wodini, nafurahi kwamba sasa nimekuwa shangazi yake, nitaendelea kumfuatilia maendeleo yake,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles