21.9 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Watoto 228 wenye ulemavu wa macho wapata bima

Allan Vicent -Tabora

WATOTO 228 wasioona na kusikia wanaosoma katika Shule ya Msingi Furaha mjini Tabora, wamekabidhiwa kadi 228 za bima ya afya iliyoboreshwa (CHF), ili kuwawezesha kupata matibabu bila malipo kwa kipindi cha mwaka mzima.

Kadi hizo zilizotolewa na Shirika la Caritas lililo chini ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Tabora, na zimekabidhiwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Komanya Kitwala.

Komanya alishukuru shirika hilo kwa moyo wao wa upendo na kuomba jamii na mashirika mengine mkoani humo kuiga tabia hiyo na kujitoa kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalumu na wasiojiweza ili kuwawezesha kuwa na afya njema.

Alisema kuwa kadi hizo ni mkombozi kwa watoto hao kwani zitawasaidia sana kuondokana na changamoto ya kukosa matibabu kwa wakati pale wanapougua kutokana na ukosefu wa fedha.

“Yeyote anayesaidia watoto kama hao anapata baraka na thawabu kubwa kwa Mwenyezi Mungu, hivyo natoa wito kwa jamii na wadau wengine wa maendeleo kuwa na moyo wa huruma kwa watoto, hasa wenye ulemavu ambao wanahitaji kusaidiwa,” alisema Komanya.

Naye Mratibu wa Bima ya Afya iliyoboreshwa Manispaa ya Tabora,  Samwel Elisante alisema jumla ya watoto wasioona 82 na wasiosikia 131 wamekabidhiwa kadi hizo na watoto 15 ambao hawajaripoti shuleni watakabidhiwa baadae.

Alifafanua kuwa kadi hizo ni za mwaka mmoja na wataongezewa muda baada ya mwaka kupita.

Komanya alibainisha kuwa zimetolewa kwa jumla ya kaya 38 zenye watoto sita sita na kila kaya imelipiwa sh 30,000.

Aliongeza kuwa kadi hizo ambazo zimegharimu Sh mil 1.14 zitawawezesha kupata matibabu katika zahanati, vituo vya afya na hospitali yoyote ile ya Serikali hapa nchini.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Furaha inayolea watoto hao, Mgisha Kashonda alimpongeza Mkuu wa Wilaya na uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kwa kuwezesha watoto hao kupata kadi za kupata huduma hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,719FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles