31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Watoto 213,000 huzaliwa njiti kila mwaka nchini

VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

WATOTO 213,000 kati ya 2,021,277 wanaozaliwa kila mwaka huzaliwa njiti na 9,000 kati ya hao hufariki dunia.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameeleza hayo leo Novemba 17 kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ikiwamo Instagram na twitter, ambapo Tanzania imeungana na mataifa mengine duniani kuadhinisha Siku ya Mtoto Njiti.

“Watoto 9,000 hufariki dunia kutokana na matatizo mbalimbali yanayohusiana na kuzaliwa ikiwamo kutopumua vizuri kwa sababu mapafu yao hayajakomaa vizuri, uambukizo na uzito pungufu,” ameandika.

Waziri Ummy ameandika “Serikali kupitia Wizara itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha watoto njiti wanahuduniwa, wanatunzwa na wanalelewa vizuri ili waishi salama.

“Nawashukuru kwa dhati watoa huduma za afya hasa wauguzi wanaowahudumia na kuwatunza watoto njiti na wadau wanaoendelea kushirikiana nasi katika eneo hili,” ameandika.

Naye Mkuu wa Idara ya Watoto, Muhimbili, Dk Mary Charles ndiye aliyefunga Kongamano la Kisayansi la Watoto Wachanga lililopewa kauli mbiu ‘Kila pumzi ni ya thamani’, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru.

Amesema takwimu zinaonyesha vifo vya watoto wachanga vimechangia kwa karibu theluthi ya vifo vyote vya watoto chini ya miaka mitano.

Amesema ili kuhakikisha hilo Muhimbili imeweka juhudi za makusudi kuhakikisha watoto wachanga wanapata huduma bora.

“Kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa tumefanikiwa kukamilisha ukarabati wa wodi ya watoto wachanga na kuwa na sakafu moja nzima itakayotoa huduma za kibingwa,” amesema Dk Mary Charles.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles