30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Watoto 20 wakutwa na matundu kwenye moyo

Dk. Sulende Kubhoja
Dk. Sulende Kubhoja

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

WATOTO 20 wamekutwa na matundu kwenye moyo baada ya kufanyiwa uchunguzi wa awali katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa watoto katika taasisi hiyo, Dk. Sulende Kubhoja alisema hayo jana alipozungumza na MTANZANIA.

“Watoto wengi huzaliwa na matatizo ya moyo lakini idadi ya wanaofikishwa hospitalini hairidhishi kulingana na ukubwa wa tatizo lenyewe.

“Hivyo tukataka waletwe   tuwafanyie uchunguzi wa awali kwa siku tatu, tangu Septemba 5, mwaka huu.

“Tumepokea watoto zaidi ya 150 wengi tumewakuta na magonjwa ya moyo lakini hawa 20 wamekutwa na tundu kwenye moyo,” alisema.

Daktari huyo alisema watoto hao watafanyiwa upasuaji hivi karibuni kuziba matundu hayo na   upasuaji huo utafanyika kwa njia ya kisasa.

“Tutaziba pasipo kufungua kifua, hii ni njia ya kisasa.

Kwa njia hii huwa tuna uwezo wa kuwafanyia watoto watano hadi 10 kwa siku.

“Pamoja na hayo bado tunaendelea na kliniki za kila siku ambako tumekuwa tukipokea zaidi ya watoto 30,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles