25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Watoto 100 wafa India kwa maradhi ya kuvimba ubongo

BIHAR-INDIA

WATOTO 100 wamekufa katika jimbo la mashariki mwa India la Bihar kutokana na maradhi ya kuvimba kwa ubongo.

Maofisa wa afya kwenye eneo hilo wamesema wanajaribu kukabiliana na ugonjwa huo hatari.

Ofisa anayeshughulikia masuala ya Afya, Sanjay Kumar amesema vifo vilivyorekodiwa tangu mwezi Juni vimetokea zaidi katika wilaya ya Muzaffarput inayotajwa kuwa kitovu cha mlipuko wa ugonjwa huo.

Msimamizi wa Hospitali katika wilaya ya Muzaffarput amesema watoto 83 walikufa katika hospitali inayomilikiwa na serikali huku wengine 17 walipoteza maisha katika hospitali ya binafsi iliyopo kwenye eneo hilo.

Wote walioathirika ni watoto wa chini ya umri wa miaka 7.

Maradhi ya kuvimba ubongo husababishwa na maambukizi ya virusi hatari vya ugonjwa huo na huongezeka wakati wa majira ya joto na msimu wa mvua ambayo mara nyingi huwa kati ya mwezi Juni na Oktoba

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles