25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Watoa matibabu ya bure kwa wanafunzi

Asha Bani – Dar es Salaam

KLABU ya Rotary ya Oysterbay jijini Dar es Salaam, wametoa za matibabu bila malipo kwa wanafunzi zaidi ya 1,500 wa shule za msingi Msasani A na B ikiwemo kuwafanyia  vipimo vya malaria, macho, ngozi, masikio, pua na koo.

Huduma hiyo ilitolewa jana katika kambi ya tiba ya siku moja iliyofanyika katika viwanja vya shule hizo ambapo wanafunzi hao wakiwa wameambatana na wazazi wao pamoja na walezi walipatiwa matibabu na ushauri nasaha kulingana na matatizo waliyokutwa nayo.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Rotary Klabu Oysterbay, Abdallah Singano, alisema lengo la kufanya hivyo ni kuisaidia jamii ambao wengi wao hawana nafasi na uwezo wa kucheki afya zao mara kwa mara.

Alisema wamekuwa wakifanya hivyo kila mwaka ambapo walifanya kambi ya Kijitonyama,Kerege Bagamoyo na Msasani kwa ufadhili wa taasisi mbalimbali zikiwemo benki ya Diamond trust  na kampuni ya kinywaji cha Sayona.

Naye Dk. Helga Mutasingwa amesema ameweza kusimamia vyema upimaji wa watoto afya zao na wengi wao wameonekana kuwa na matatizo ya ngozi,masikio na koo .

“Naamini katika matatizo ya ngozi kumesababishwa kutokuwa na lishe bora ,hawazingatiwi usafi pamoja na kula matunda,Protein na Vitamin ,lakini pia ushauri na utoaji wa elimu unatakiwa kuzingatiwa wakati wote,’’alisema Dk.Helga.

Alisema wangependa kama klabu kufanya hivyo katika maeneo mbalimbali ya shule na mikusanyiko ya watoto lakini kutokana na kutokuwa na uwezo wa wafadhili wamekuwa wanachagua maeneo machache kufanya hivyo.

Naye  Rais wa Klabu hiyo, Amish  Shah alisema kambi hiyo ya huduma za afya ni moja kati ya misaada mbalimbali wanayoitoa kwa ajili ya kuzisaidia shule hizo ambapo mbali na huduma, wanafunzi hao hupatiwa dawa, vifaa vya usafi zikiwemo taulo za kike kwa ajili ya kusaidia hedha salama, vyakula pamoja na maji.

Aidha alisema huduma nyingine walizozitoa katika kambi hiyo ni pamoja na vipimo na tiba za meno, minyoo pamoja na kuwapatia miwani wanafunzi watakaogundulika kuwa na tatizo la macho.

“Kambi ya huduma za afya ni mfano mmoja mkubwa unaoonyesha namna ambavyo wanachama wa Rotary wanavyozihudumia jamii zao, misaada ya miradi midogo inayohitajika zaidi hutolewa kwa njia ya fedha pamoja na kazi za kujitolea. Misaada hyo hutolewa na watu wanaotaka kuleta mabadiliko katika jamii”  alisema.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles