25 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

WATOA HUDUMA MSALABA MWEKUNDU WAPUNGUA

NA GUSTAPHU HAULE, PWANI

CHAMA cha Msalaba Mwekundu Mkoa wa Pwani, kimewashauri wananchi mkoani humo kuendelea kujiunga na chama hicho ili waweze kusaidia jamii katika kukabiliana na  majanga mbalimbali yakiwamo mahitaji ya damu salama.

Mratibu wa chama hicho Mkoa wa Pwani, Estrider Pallingo, alitoa wito huo juzi kwenye maadhimisho ya chama hicho yaliyofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Tumbi.

Maadhimisho hayo pia yalikwenda sambamba na kuchangia damu pamoja na kutoa msaada wa vifaa vya kinga mikononi.

Pallingo alisema maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka duniani kote lakini kwa Mkoa wa Pwani walifanyia katika Hospitali ya Tumbi kwa kuwa wanatambua imekuwa msaada mkubwa kutokana na ajali zinazotokea katika barabara ya Morogoro.

Alisema Msalaba Mwekundu inawafikia watu wenye matatizo na majanga mbalimbali ikiwemo wale wanaohitaji msaada wa kuongezewa damu na wakati mwingine inawawia vigumu kutimiza matakwa hayo kutokana na uchache wa wanachama waliopo.

“Leo tunaadhimisha siku ya redcross duniani lakini bado tuna changamoto kubwa ya watu kushindwa kujiunga na chama hiki, tunaomba mjitokeze kwa wingi ili tuweze kuwasaidia wahanga wanaopata matatizo mbalimbali hasa ya damu,” alisema Pallingo.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Tumbi, Edward Wayi, alisema siku ya msalaba mwekundu duniani ni muhimu kwa mataifa yote kwa kuwa yanalenga kuhamasisha jamii namna ya kusaidiana katika matatizo.

Aidha, Wayi alikishukuru chama hicho kwa kutambua umuhimu wa kufanyia maadhimisho hayo hospitalini hapo na kusema kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano kwa chama hicho katika kutatua matatizo ya jamii.

Naye Mwahamasishaji wa kitengo cha damu salama kilichopo katika Hospitali ya Tumbi, Feliciana Mmasi, alisema jumla ya chupa 15 za damu zilipatikana katika maadhimisho hayo huku akisema mahitaji ya damu kwa siku katika hospitali hiyo ni chupa 20.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,624FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles