28.9 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

Watendaji Tasaf Pwani watakiwa kuonyesha uhalisia wa kinachofanyika

Na Upendo Mosha, Pwani

KATIBU Tawala Mkoa wa Pwani, Rashid Mchatta, amewaelekeza watendaji wanaohusika na Mpango wa kunusuru kaya masikini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kuhakikisha wanaonyesha hali halisi ya kile kinachofanyika kwenye maeneo yaliyolengwa.

Mchatta ametoa maelekezo hayo June 26,2024 alipokuwa akifungua kikao kazi kilichofanyika Mjini Kibaha ambacho kilikuwa kinajadili taarifa ya utekelezaji wa mpango huo kwa mkoa wa Pwani.

Katibu Tawala huyo amesema tathmini ya utekelezaji wa mpango wa TASAF inatakiwa kuonekana na kwenye maeneo yanayotekelezwa Mpango huo kwa kuona mabadiliko kwa walengwa.

“Mkitembelea kwenye maeneo ya mpango mnatakiwa kuonyesha nini kimefanyika Ili maeneo mengine waone namna Mpango huo ulivyotekelezeka na kuleta matokeo chanya kwa walengwa,” amesema.

Mkurugenzi wa Uratibu wa TASAF, Haika Shayo, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TASAF, amesema wamefanya ziara katika Mkoa wa Pwani kuona utekelezaji wa mpango kwa walengwa wakiambatana na wadau wa maendeleo

Amesema ili uendelea kuwainua wanufaika katika shughuli zao za kiuchumi ni vema wakaunganishwa na Shirika la viwanda vidogovidogo iwe rahisi kwao kutangaza bidhaa zao na kupata wanunuzi.

Mratibu wa wa TASAF Mkoa wa Pwani, Roseline Kimaro, amesema kupitia Mpango huo wanufaika wamekuwa na mabadiliko ya kiuchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles