22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

Watendaji Halmashauri ya Chemba watajwa chanzo cha kupata hati yenye shaka

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Watendaji wa Halmashauri ya Chemba mkoani Dodoma wametajwa ndio chanzo cha halmshauri hiyo kupata hati yenye mashaka kutokana na kuwepo kwa upungufu katika ufungaji wa mahesabu ambapo inadaiwa baadhi wamekuwa hawapeleki fedha benki pamoja na baadhi ya nyaraka kutoonekana.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Said Sambala wakati akizungumza katika kikao cha kujadili hoja zilizoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Kikao hicho kimehudhuriwa na madiwani na watendaji wa H]halmshauri hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Dk. Semistatus Mashimba, Mkuu wa Wilaya, Simon Chacha, Afisa Utumishi wa Mkoa wa Dodoma na baadhi ya watendaji kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

Mwenyekiti huyo huyo amesema Halmashauri hiyo kupata hati yenye mashaka inamaana kwamba kuna baadhi ya watendaji hawatimizi wajibu wao kwani hali hiyo imekuwa ikijitokeza kila ikitoka ripoti ya (CAG) hivyo kuna watu wanatakiwa kuwajibishwa.

“Halmashauri yetu imekuwa ikisongwa na mambo madogo madogo ifike mahala tusimamie vizuri haya mambo kila siku sisi tu tunafanyaje kutoka katika hii hali,”amesema Mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Abdi Msuri ambaye ni diwani wa Jangalo amewataka watendaji wote waliopewa dhamana ya kukusanya mapato ya ndani ya halmashauri kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia sheria, uaminifu na uadilifu wanapo tekeleza jukumu hilo, huku akionya kwamba wale wote watakaokwenda kinyume wata ondolewa katika nafasi hizo.

“Tumeomba sana tuwe pamoja lakini kama vile hatuendi kawaida,wakuu wetu hawana itifaki kabisa sasa itabidi tuchukuliane hatua hatutakuonea ila tutakutendea haki,ni uzembe ni uzembe ni uzembe…tuende kama timu kila mmoja awajibike mnasema eti wale ni wanasiasa iko siku utaona madhara  ya hao wanasiasa,”amesema Msumari.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Chacha amesema kila mwaka kuwa na upungufu katika ufungaji wa mahesabu huo ni uzembe hivyo amemwagiza  Mkururugenzi wa Halmashauri hiyo, Dk Mashimba kuwasimamia watendaji wote kwa kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake.

Naye, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Dk. Mashimba amesema awali walikuwa wakikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa watendaji lakini kwa sasa imetatuliwa na katika baadhi ya kada tayari wameishafika hivyo kwa sasa watafanya kazi kwa weledi ikiwa ni pamoja na kufunga mahesabu kwa wakati pamoja na kuhifadhi nyaraka muhimu.

“Ole wako ukae na hela ya Serikali nyumbani kwako tunataka upeleke benki.Mmabo mengine yote tutayaweka vizuri tayari tumepata watu wenye weledi,”amesema.

Kwa upande wake, Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Salome Singano amesema hataki kuona tena jambo hilo linajitokeza katika Halamshauri hiyo huku akisiitiza umuhimu wa kila manunuzi kuwekwa katika  nyaraka  ikiwemo kuwemo kwa chumba maalum cha kutunza nyaraka.  

Naye, Mkaguzi Mkuu wa Nje Mkoa wa Dodoma kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali,Chambi Sasamka ameliomba Baraza la Madiwani kuwasimamia watendaji wa Halmshauri hiyo kwani wamekuwa wakifanya makosa ya kizembe ikiwemo kutokuwasilisha vitabu vyenye uhalisia.

Mkaguzi huyo amesema sasa ni wakati wa watendaji hao kuzingatia muongozo wa ufungaji  wa mahesabu ili Halmshauri hiyo isiwe kila mwaka inapata hati yenye mashaka.

“Kupata hati yenye mashaka sio kwamba kuna wtu wamekula hela mfano hapa ni baadhi ya nyaraka hazijaonekana lakini wengine kutokupeleka fedha benki sasa haya ni lazima yaangaliwe ili yasijitokeze tena,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles