28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Wateja wa Tigo na Zantel kunufaika na muungano wa kampuni hizo

Na mwansishi wetu

wateja wa kampuni za simu za mkononi ya Tigo na Zantel wameanza kufurahia muungano wa kampuni himzo, ambazo zimemeungana mapema mwaka huu.

Mapema mwaka huu wakurugenzi wa kampuni hizo mbili waliweka bayana
kusudio hilo la kuungana katika mahojiano na jarida maarufu duniani
la Forbes toleo maalumu la kujenga Tanzania yenye mafanikio na baada ya kuungana watenga wameanza kunufaika na huduma zinazotolewa na kampuni hizo.

Jarida hilo lilisema wateja walionufaika ni kutoka katika maeneo mawili ambayo ni Tanzania bara na visiwani na kutaja baadhi ya huduma ambazo wananufaika kuwa ni bei nafuu ya miingiliano ya simu, huduma ya tigopesa na easypesa, bando, data pamoja na huduma nyinginezo ambazo zinatolewa na kampuni hizo.

Katika mahojiano hayo, wakurugenzi wa kampuni hizo Waliweka wazi namna gani muungano huo utaleta faida kwa wateja wa kampuni hizo mbili kupitia kuboresha huduma kwa kiwango cha juu na sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi kwa ujumla.

Katika mahojiano hayo wakurugenzi hao walisema wateja walionesha wasiwasi kuhusu muungano huo na faida zake lakini waliwahakikishia kuwa kutokana na kuunganisha nguvu kwa kampuni hizo wateja watafurahia huduma kwani teknolojia imepanuka zaidi hivyo kuweza kutoka huduma katika ubora wa hali ya juu.

Walisema muungano huo unaleta nguvu za kampuni zote mbili pamoja na kutoa kilicho bora zaidi kote bara na visiwani, mijini na vijijini. Pia utaongeza wigo wa kufanya biashara toka pande zote mbili, pia waliwataka wateja wao kufahamu kuwa mbali na wateja wa Tigo na Zantel kufaidika pia hata wale wa mitandao mingine pia watanufaika na muungano huo katika sekta mbalimbali ikiwemo uchumi na mawasiliano.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Tanzania Simon Karikari alikaririwa akisema anaamini muungano huo utatengeza sekta bora zaidi ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini Tanzania kwa sasa na siku za usoni, na kuongeza kuwa soko lenye kampuni zilizoungana kama hivi litasukuma mbele ubunifu.

Mbali na wakurugenzi hao pia Wataalamu wa uchumi na teknolojia wameweka bayana athari hasi za kuwa na soko vipande vipande au lenye kampuni nyingi za mawasiliano ya simu za mkononi ambazo hazijaungana watashindwa kuwa na ufanisi na kushindwa kuwekeza mitaji mikubwa yenye kukuza tija kwa mtumiaji kwa muda mrefu.

Wataalamu hao walisema muungano wa Tigo na Zantel ni hatua kubwa na muhimu katika kukuza sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini Tanzania na kuleta mabadiliko chanya katika sekta hii.

Hivi Sasa zimebaki kampuni tano badala ya sita kutokana na kuondoka kwa kampuni ya Smart mwezi jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles