26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wateja kumbi za starehe kukaguliwa

Na Brighiter Masaki

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amewataka wamiliki wa kumbi za starehe kuanza kuwakagua wateja wanaoingia kwenye kumbi hizo ili kujua kama wamebeba silaha.

Simbachawene  ametoa maagizo hayo leo,  wakati wa ziara yake wilayani Mufindi mkoani Iringa baada ya tukio la mauaji kwa kutumia silaha yaliyotokea hivi karibuni  jijini Dar es Salaam.

 Waziri huyo amesema kuwa wamiliki hao wanatakiwa kuanza kuwapekua wateja wao ili kupunguza matumizi mabaya ya silaha hapa nchini.

Simbachawene amefafanua kuwa mtu anayetakiwa kupewa silaha lazima aangaliwe uwezo wa akili yake, kama ana karoso yoyote katika ubongo wake wakati anakua hadi  kufikia umri wa utu uzima.

 “Kwa sasa imejitokeza vijana wanafiriki kumiliki silaha sawa na cheni ya dhahabu wanakuwa wanataka akifika sehemu kila mtu ajue kama yeye anamiliki silaha lakini mtu ambaye anatakiwa kumiliki silaha ni yule ambaye anakuwa na tishio la kiusalama au anadhani kutokana na shughuli ambayo anaifanya anahitaji kumiliki silaha,” amesema Simbachawene

 Pia ameeleza kuwa adui yako hapaswi kujua kama unamiliki ili akitaka kukudhuru ajue tu nawe uwezo wa kujilinda na kijikinga kwa kutumia kifaa hicho.

“Kwa sasa ni tofauti, mtu anaenda baa anaonyesha silaha huo unaitwa ni ushamba na ukiukwaji wa sheria za umiliki wa silaha kutokana na hali hii niliagiza jeshi la polisi muda kama mwezi umepita kazi kubwa sana inafanyika na ripoti yake ya awali imeletwa ofisini kwangu ya namna ya mianya ya umilikishaji wa silaha unavyofanyika,” amesema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles