27.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Watatu wafariki dunia D’Salaam

Dar es Salaam
Eneo la katikati ya Jiji la Dar es Salaam

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

WATU watatu wamefariki dunia katika matukio matatu tofauti likiwamo la mtoto Jackline Lubaka (5), kufariki baada ya ukuta kumdondokea.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kihenya Wakihenya, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 11 jioni wakati Lubaka alipokuwa akicheza na wenzake pembezoni mwa nyumba wanayoishi ghafla alidondokewa na ukuta na kufariki dunia papo hapo.

Alisema chanzo cha ajali hiyo ni uchakavu wa nyumba hiyo, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke na upelelezi bado unaendelea.

Katika tukio jingine, mwendesha bodaboda yenye namba za usajili T385 BNS, Riziki Abdul (17) ambaye ni mkazi wa Saku Mbagala, amefariki dunia papo hapo baada ya kugonga mti wa mnazi wakati alipokuwa akiendesha pikipiki hiyo.

Alisema tukio hilo lilitokea juzi saa sita usiku katika Barabara ya Saku eneo la Saku Container na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke.

Katika tukio jingine, mwanaume ambaye hakufahamika (35 – 40), amekutwa amefariki dunia katika eneo la Mbweni Malindi ufukweni mwa Bahari ya Hindi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 11 alfajiri baada ya mwili wa mtu huyo kukutwa ukiwa umeharibika na kushindwa kutambuliwa.

Alisema maiti hiyo ilifanyiwa uchunguzi papo hapo na kuzikwa katika eneo hilo na hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles