Watatu wafa maji Manyara

0
1236

Mohamed Hamad, Simanjiro

Watu watatu katika Kijiji cha Korongo, wilayani Simanjiro mkoani Manyara, wamepoteza maisha baada ya kuzama kwenye maji wakati wakivuka kutoka eneo moja kwenye jingine kijijini hapo.

Waliofariki ni Abudiela Mohamedi Hela (50), Hamadi Bashiri Mwiru (30) na Haji Abduli (33).

Tukio hilo limetokea leo Ijumaa Mei 15, baada ya mtumbwi waliokuwa wamepanda kupinduka na kusababisha watu hao kuzama ambapo walipatikana baadae wakiwa wote wamefariki.

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, Zephania Chaula amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema chanzo cha vifo hivyo ni ulevi kwa watu hao ambao ulifanya washindwe kuvuka kisha kuzama.

“Juzi tu nilikuwa hapo nikiongea na wananchi, nilitoa tahadhari nikiwataka wawe makini na mvua zinazoendelea kunyesha, wasivuke maji mengi kwenye maeneo yenye maji yanayotiririka kwa wingi wakiwemo watoto wadogo,” amesema Chaula.

Amesema mwili mmoja wa marehemu hao umeshakabidhiwa ndugu na umezikwa, huku mingine miwili ikisubiri ndugu zao kwaajili ya taratibu
zaidi za mazishi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here