25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania watakiwa kuchangamkia fursa vyuo vya nje

FARAJA MASINDE

WATANZANIA  wametakiwa kuchangamkia fursa  katika vyuo vya elimu ya juu nje ya nchi ili kupata ujuzi  unaoendana na  mabadiliko ya haraka ya teknolojia.

Wito huo umetolewa jana Dar es Salaam na Mwambata wa Mwenza  wa Taasisi ya Elimu ya Juu ya Edugate  ya Uingereza,   Aliyuthuman  Sadhique, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi  wa program  maalumu ya kusaidia wanafunzi katika nchi zenye uchumi wa kati  inayofahamika kama LICAP.

Alisema program hiyo  inalenga kuwafikia  wanafunzi na wahitimu  mbalimbali kutimiza malengo  katika vyuo maalumu vilivyopo Uingereza na Sri Lanka.

“Edugate kwa kushirikiana na Taasisi ya  British Colledge  of Upplies  Studies ya Sri Lanka tumedhamilia kuwekeza  katika elimu hapa nchini hususan kuwawezesha watanzania kwenda kusoma nje  ya nchi ikiwemo kuwasaidia  kimasomo,”alisema.

Aidha, leo Januri 25,  katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, itazinduliwa program hiyo ambapo uzinduzi utaaendana na kongamano maalumu litakalo toa fursa kwa watanzania kuzitambua fursa hizo za elimu.

Sadhique alisema  kongamano  hilo halitakuwa na  malipo yoyote na mtu yoyote anaweza kuhudhuria  hususan wenye nia ya dhati ya kwenda kujiendeleza nje ya nchi.

Aliwataka wale wote wenye nia ya kusoma  nje ya nchi kuhudhuria  kongamano hilo na kwamba litakuwa na faida kubwa  hususan kwa wahitimu wa Teknolojia ya habari na Mawasiliano (IT), Usimamizi wa fedha, uhandisi  na taaluma zingine .

Alisema  kwa wale ambao ufaulu wao utaonekana kuwa ni wajuu  watasaidiwa kupata  udhamini  kupitia program hiyo  ya  LICAP.

Mmoja wa waratibu wa kongamano hilo David Munanka, alisema, mafunzo hayo  yamekuja wakati muafaka ambapo serikali ya awamu ya tano inatekeleza dira yake ya kuelekea uchumi wa viwanda.

“Yeyote  mwenye sifa  na nia ya kusoma shahada au astahashada nje ya nchi anaweza kuhudhuria kongamano hili bure,”alisema Munanka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles