Watanzania watakiwa kuchangamkia bima ya Ajali na Maisha kwa kununua mafuta

0
675

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

WATANZANIA hususan wamiliki wa vyombo vy moto ikiwamo gari, bajaji na pikipiki wametakiwa kuchangamkia fursa ya bima ya ajali na maisha ambapo kwa kujiunga na huduma hiyo wateja wote watakaolipia mafuta kuanzia Sh 10,000 kupitia Selcom Pay Mastercard QR au kadi ya Puma kwenye vituo vya Puma Energy vya Dar es Salaam watanufaika na bima hiyo.

Wakurugenzi wa makampuni ya Puma energy Tanzania, Selcom Tanzania, Sanlam pamoja na Tanmanagement Insurance Brokers Limited wakisaini mkataba wa makubaliano ya kuanzisha huduma ya Bima ya ajali na maisha ambayo italenga kuinua sekta ya soko la bima Tanzania. Kuuanzia kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Sanlam Tanzania, Khamis Suleiman,Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom Tanzania, Sameer Hirji Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mafuta ya PUMA Energy Tanzania, Dominic Dhanah na Mkurugenzi Mtendaji wa TanManagement Insurance Brokers Limited, Mohammed Jaffer.

Bima hiyo inakuja ikiwa ni baada ya kuungana kwa wadau wakuu wanne katika sekta ya bima, technolojia na huduma za kifedha, na nishati lengo ambao ni Puma Energy Tanzania, TanManagement Insurance Brokers, Selcom Tanzania na Sanlam Tanzania likiwa ni kuinua sekta ya soko la bima nchini. 

Hii ina maana kwamba mteja anapojiunga na mfumo huo basi atapokea bima ya Ajali na Maisha itakayotumika ndani ya siku sab ana pindi inapotokea amepata amepoteza Maisha atalipwa Sh 1,000,000 kiwango sawa na akipata ulemavu huku akipata ajali wakati akitumia chombo cha moto atalipwa Sh milioni 2 ndani ya saa 24.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Septemba 13, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania, Dominic Dhanah, amesema kuwa imekuwa ni ndoto yao ya muda mrefu katika kuhakikisha kuwa wanawasaidia Watanzania katika kupata huduma muhimu na zilizoboreshwa na kwamba maisha ya wateja wao ni jambo wanalolipa kipaumbele zaidi.

“Puma Energy Tanzania Limited ikiwa ni kampuni namba moja ya mafuta Tanzania na kampuni inayo ongoza kwenye sekta ya mafuta kwa kutoa masuluhisho ya kidijitali kwa wateja wake, sikuzote imekuwa ikijitahidi kushirikiana na makampuni yenye mtazamo kama wetu kuboresha ubora wa huduma zitolewazo kwa wateja wetu. 

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mafuta ya PUMA Energy Tanzania, Dominic Dhanah, akizungumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa ya kipekee ya Bima ya ajali na maisha ambayo italenga kuinua sekta ya soko la bima Tanzania.Uzinduzi huo umefanyika Septemba 13, jijini Dar es Salaam.

“Huduma hizi za bima ya maisha kwa wateja wetu ni moja jitihada hizo chanya. Kupitia mpango huu wateja wetu sasa wataweza kupata bima za maisha bila ya gharama ya ziada watakacho takiwa kufanya ni kulipia mafuta yao kidijitali kupitia mfumo wa selcom. Huduma hii ina akisi maudhui ya kampuni yetu ambayo ni kuchagiza maendeleo chanya kwenye jamii zinazotuzunguka, hivyo kinga ya bima hii itatolewa wakati halisi na haina kipindi cha kusubiri,” amesema Dhanah.

Akifafanua zaidi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Tanzania, Khamis Suleiman, amesema kuwa wameamua kutafsiri kwa vitendo maelekezo ya Wizara ya Fedha na Mipango katika kuhakikisha kuwa wanafikia asilimia 50 ya watu wazima Walid angalau na aina moja ya bima ifikapo 2028.

“Tunatafsiri kwa vitendo maelekezo ya wizara ya Fedha na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima ya kufikia lengo la asilimia 50 ya watu wazima walio na angalau aina moja ya bima ifikapo mwaka 2028, kuongeza mchango wa tasnia ya bima kwenye pato la Taifa kufikia asilimia 5. Malengo haya pia yana dhamira ya kupunguza umasikini kwa kutoa fidia kwa wale waliotharika, hakutakuwa na gharama ya ziada kwa mbima katika utaratibu huu.

“Huduma hii itawahusu Wateja ambao hununua Mafuta mara kwa mara kwenye vituo vya Puma Energy vya Dar es Salaam, kwa njia ya kidigitali katika hatua nyingine ambayo imehimizwa na Serikali kupunguza matumizi ya pesa taslim katika kukuza ujumuishaji wa kifedha,” amesema Suleiman.

Upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Selcom Tanzania, Sameer Hirji, amesema wao kama kinara kwenye nyanja ya mifumo ya malipo nchini kwao ni heshima kuona ni kwa namna gani wanasaidia kuendelea kuhimiza matumizi ya kidigitali nchini.

“Tukiwa waongoza njia katika mifumo ya malipo hapa Tanzania, ni heshima kuendeleza juhudi zetu za kupunguza pengo la kidigitali sokoni. Mchakato huu utatumia teknolojia ya kisasa kabisa kuhakikisha kwamba tunafikia lengo la kufikisha huduma ya Bima kwa watu wengi iwezekanavyo. Selcom inakuja ikiwa na kanzidata ya wateja katika ncha ya chini kabisa ya mnyororo, jambo linalotoa nafasi kwa juhudi za wadau wetu kufika wa wateja hawa bila gharama ya ziada.

“Ushirikiano wetu na Sanlam, Puma na TanManagement unathibitisha wajibu wa viongozi katika sekta husika kwenye kuhakikisha ulinzi wa jamii na uboreshaji wa ustawi wa wateja wetu, na jamii nzima kwa ujumla,” amesema Hirji.

Mkurugenzi Mtendaji wa TanManagement Insurance Brokers Limited, Mohammed Jaffer, akizungumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa ya kipekee ya Bima ya ajali na maisha ambayo italenga kuinua sekta ya soko la bima Tanzania.Uzinduzi huo umefanyika Septemba 13, jijini Dar es Salaam.

Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa TanManagement Insurance  Brokers Limited, Mohammed Jaffer, amesema hiyo itakuwa ni aina ya kwanza aya bima kutolewa nchini kwa mfumo nchini na kuhimiza watanzania kuchangamkia fursa hiyo ili kuwa na uhakika.

“Hatutarajii iwe ya mwisho. dira yetu ni kupanua huduma hii katika vituo vingine vya mafuta na pia kulenga maeneo mengine ambayo yatamnufaisha mteja, bima inapaswa kufanywa kuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku, iwe kwa kukata bima moja kwa moja au kunufaika kupitia huduma nyingine. Tunataka bima iwe moja ya mahitaji ya msingi, kwasababu siku hizi inashauriwa kuwa na angalau aina moja ya Bima. Lengo letu ni kuhakikisha tunafikisha huduma hii kwa watanzania kupitia njia hizi mpya. Tumejipanga na tunatarajia kufanya zaidi!,” amesema Jaffer.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here