26.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania wasiwe na hofu kuhusu vitambulisho kuisha muda-NIDA

*Yasema kinachobadilishwa ni picha tu

Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital

MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa( NIDA) imesema kuwa licha ya vitambulisho vya Taifa vya mwaka 2012 kuonesha vinaisha muda wake imewatoa hofu wananchi na kuwataka kutambua kuwa utambulisho wao utabaki palepale.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 46 ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Msemaji wa Mamlaka hiyo, Geofrey Tengeneza amesema kinachokwenda kuisha muda wa matumizi ni kibebeo cha kitambulisho lakini utambulisho wa mwanachama unabaki palepale .

Amesema huduma zote ambazo wamekuwa wakizipata kupitia kitambulisho hicho au namba ya kitambulisho zitabaki kuwa palepale licha ya muda wa kitambulisho kwenda kuisha 2023.

“Licha ya kwenda kuisha kwa muda wa matumizi ya kibebeo cha kitambulisho cha taifa naomba wananchi mjue kuwa utambulisho wa mwananchi unabaki palepale na auishi muda wa matumizi,” amesema Tengeneza.

Kwa mujibu wa Tengeneza, kinachokwenda kufanyika baada ya muda kuisha muda wa kitambulisho mwananchi atapaswa kwenda katika ofisi ya wilaya katika eneo ambalo anaishi kufika pale kwa ajili ya kupigwa picha.

“Zoezi ambalo litafanyika ni kupiga picha tu hakutakuwa na hatua uhakiki wa taarifa zako na baada ya hapo NIDA tutaendelea utaratibu wa kuandaa kanzi data yetu,” amesema Tengeneza.

Aidha, amebainisha kuwa matumizi ya kitambulisho cha taifa yamekuwa ni ya miaka 10 lengo likiwa ni kufanya mabadiliko ya taarifa za Wananchi tofauti na zile ambazo alitoa awali.

Akitaja sababu za kufanya mabadiliko ndani ya miaka 10, Tengeneza amesema inawezekana mtu akawa amebadilisha makazi ya awali hivyo ni lazima taarifa zake zikahuishwa katika mfumo wa kanzi data.

Pia amefafanua kuwa katika muda wa miaka 10 muonekano wa mtu unaweza ukawa umebadilika, hivyo katika kipindi hiki ni lazima afanye mabadiliko .

“Hizi ndizo sababu ambazo kwanini tumeweka muda wa miaka 10 nawaomba Watanzania wasiwe na hofu yoyote Wala kuhusu foleni pindi mchakato utakapoanza wa kupiga picha hakutakuwa na foleni ya aina yoyote endapo hatakuwa na taarifa za kuhusisha,” amesema.

Vilevile alisema vitambulisho hivyo ambavyo ni vya mwaka 2012 avitakuwa vikiisha muda mmoja na badala yake vinaisha kwa muda tofauti kulingana na tarehe na mwezi na mwaka hivyo wananchi wasiwe na hofu kuhusu suala la foleni.

Aidha, amesema NIDA imejipanga kutoa huduma hiyo kwani tayari imekwisha toa oda ya vifaa vipya kwa ajili ya zoezi hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles