24.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania tuchanje chanjo ya Uviko-19-Majaliwa

Na Faraja Masinde, Mbeya

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amehimiza Watanzania kuendelea kuchanja chanjo ya Uviko-19 huku akisisitiza kuwa chanjo siyo laima ila ni muhimu.

Majaliwa ametoa wito huo Ijumaa Novemba 26, wakati akifungua Kongamano la Kisayansi la Kitaifa Kuhusu VVU na UKIMWI katika Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kwenye ukumbi wa Hoteli ya Mbeya Modern Highland , jijini Mbeya. Kaulimbiu ya Kongamano hilo inasema “Zingatia Usawa, Tokomeza Ukimwi, Tokomeza Magonjwa ya Mlipuko”.

Rais Samia Suluhu akipata Chanjo ya Uviko-19

Amesema iwapo chanjo ya Uviko-19 ingekuwa na madhara basi Rais Samia Suluhu asingekubali kuchanja na kwamba ndio maana aliunda jopo la wataalamu kwa ajili ya kuchunguza aina hizo za chanjo na wakaleta majibu.

“Niwakumbushe Watanzania wenzangu kuwa pamoja na kupambana na janga hili la UKIMWI lakini nataka tufahamu kuwa Uviko-19 bado upo, hivyo ni muhimu kila mmoja wetu hakikishe kuwa anapata chanjo ya uviko.

“Kwani sote tuliona Rais wetu Samia Suluhu alijitokeza mbele ya umma na kuchanja, hivyo iwapo chanjo hizi zingekuwa na madhara basi yeye kama kiongozi asingekubali kufanya hivyo.

“Lakini niwakumbushe tu kwamba rais aliunda tume ya Wataalam wetu ambao wote ni Watanzania wakaenda kuchunguza na wakatuletea majibu, hivyo hili litupe msukumo wa kuziamini chanjo hizi,” amesema Majaliwa.

Kwa mujibu wa Serikali Chanjo ya Uviko -19n bado ipo ya kutosha, hivyo ni muhimu kwa kila mmoja kupata cfhanjo hiyo ili kujikinga na janga la Uviko -19.

Aidha, amesisitiza kuwa iwapo mtu atapata chanjo hizo hata pata shida kama ambavyo ilikuwa ikipotoshwa na baadhi ya watu.

“Binafsi nimepata chanjo hii ya Uviko-19 na niko salama nimeendelea kufanya mazoezi sisumbuliwi na chochote na nachapa kazi kama kawaida.

“Hivyo twendeni tukachanje uzuri kwa sasa kuna chanjo za kila aina, lakini isije ikatafrika kuwa Waziri Mkuu amelazimisha watu kuchanja hapana, chanjo siyo lazima ila ni muhimu,” amesema Majaliwa.

Ikumbukwe kuwa Mkoa wa Mbeya ni kati ya Mikoa mitatu iliyofanya vizuri kwenye eneo la utoaji wa chanjo ya uviko nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles