22.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania sasa kupiga kura popote

 Damian Lubuva

Damian Lubuva

Jonas Mushi na Christina Gauluhanga, Dar es Salaam

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), inaangalia uwezekano wa kisheria kuruhusu Watanzania kupiga kura sehemu yoyote nchini tofauti na ilivyo sasa ambapo lazima upigie pale ulipojiandikishia.

Akizungumza katika Maonyesho ya 40 ya Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Damian Lubuva, alisema wamepokea maoni hayo hivyo wataangalia namna bora ya kurekebisha sheria ili iruhusu wananchi kupata fursa ya kupiga kura katika eneo lolote nchini.

Alisema sheria ya sasa inaangalia sehemu mtu alipojiandikisha katika kituo jambo ambalo wameona lina upungufu hivyo kunahitajika maboresho ili uchaguzi ujao liwekwe wazi.

Alisema katika maonyesho hayo wananchi wamepata fursa ya kujifunza shughuli za NEC ikiwa ni pamoja na kupata elimu ya mpigakura na mengineyo.

Alisema uchaguzi uliopita umemalizika kwa amani na kuwasilisha ripoti na sasa wanajiandaa na uchaguzi unaokuja.

 

Alisema kuna mambo wanayojielekeza kama suala la uandikishaji kwani katika mfumo wa BVR sasa wamepata kanzidata, hivyo siku zijazo wataandikisha watu wote waliofikisha umri wa kupiga kura na kuwaondoa katika daftari la kupiga kura waliofariki dunia.

 

Alisema katika uchaguzi ujao wanaanza uandikishaji na wanataka kuwa endelevu bila kusubiri kipindi cha uchaguzi tu huku wakiangalia uwezekano wa kuwa na watu wao katika halmashauri zote nchini.

Kuhusu Tume huru ya uchaguzi, Jaji Lubuva alisema wengi wanadhani kuwa tatizo ni kwakuwa mwenyekiti wake anateuliwa na Rais ambaye ni kiongozi wa chama fulani cha siasa na kudhani lazima atapendelea chama chake huku akisisitiza kuwa jambo la muhimu ni usimamizi na utendaji kazi bila kuingiliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles