28.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 25, 2021

WATANO WAKAMATWA KWA NYAVU HARAMU SENGEREMA

 

 

Na JUDITH NYANGE,

JESHI la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu watano kwa kupatikana na nyavu za makokoro wilayani Sengerema.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, alisema watuhumiwa hao walikamatwa katika Kijiji na Kata ya Nyarwambo wilayani  ya Sengerema.

Alisema  watu hao walikamatwa  na  askari waliokuwa katika doria  ambao walipokea taarifa kutoka kwa raia wema kwamba katika maeneo Kijiji cha Nyarwambo kuna  watu wanaojihusisha na uvuvi haramu.

Kamanda Msangi alisema askari waliweza kuwakamata watuhumiwa watano wakiwa na makokoro mawili yakiwa kwenye mtumbwi.

“Watuhumiwa waliokamatwa katika msako huo  ni Poneja Mkashi (51) mkazi wa Kijiji cha Ngoma B, Simeo John (23), Mashaka Hitila (17) naDaniel Lucas (25), wote   wa Kijiji cha Rubanda,  na Turuzira Hitila (35) mkazi wa Kijiji cha  Kahumuro,” alisema Kamanda Msangi.

Alisema watuhumiwa wote wanahojiwa na polisi  na uchunguzi ukikamalika watafikishwa mahakamani.

Kamanda alisema upelelezi na msako kuwatafuta watu wengine wanaojihusisha na uvuvi haramu katika maeneo yote unaendelea.

  Msangi amewataka  watu wote wanaojihusisha na shughuli za uvuvi kufanya kazi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na serikali.

Ppia amewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu mapema waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,099FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles