24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Watano kizimbani kwa tuhuma za utapeli

PATRICIA KIMELEMETA-DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imempandisha kizimbani Mkurugenzi wa Kampuni ya VKP Investment Four Youth, David Manot na wenzake watano na kusomewa mashtaka 32 likiwamo la kula njama na kujipatia zaidi ya Sh milioni 300 kwa njia ya udanganyifu.

Wakili wa Serikali, Ester Martin aliwataja washtakiwa wengine mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mmbando kuwa ni mwanasheria wa kampuni hiyo, Ernest Ngonyani, mfanyabiashara Yona Kiita, Mkurugenzi wa Masoko, Jane Isack, Ofisa Masoko Modikai Kilala na Meneja Uendeshaji, Juliana Kasambala.

Wakili Ester alidai kuwa washtakiwa hao walitenda makosa hayo kati ya Januari 2016 na Desemba 2018 katika jengo la Mwalimu House lililopo Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.

Washtakiwa hao wanadaiwa kula njama ya kutenda kosa la kujipatia zaidi ya Sh milioni 300 kwa njia ya udanganyifu.

Katika shtaka la kwanza la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, washtakiwa wote wanadaiwa kati ya Novemba 21, 2017 na Aprili mahali hapo hapo, kwa nia ya kutenda kosa walijipatia fedha kupitia kampuni hiyo kutoka kwa Anna Kavishe kwa kujifanya kuwa wangemuuzia kiwanja huku wakijua kuwa si kweli.

Washtakiwa hao wanadaiwa kupata kiasi tofauti tofauti cha fedha kutoka kwa Joel Olinda, Mlolu Chelehan, Shukuru Olomi, Emmanuel Mlambity, Agnes Joseph,  Christopher Mraha, Prowin Mtei, Mustapha Ngayoma,Chausiku Kinyehe, Issa Illy, Samson Ngayoma, Asha Mtangaza, Prisca Mrope Dotto Pangimoto, Nice Mohammed, Elizabeth Makombe na Elirehema Mangore.

Wengine ni Mgaza William, Nataka Milivya, Joyce Chacha, Diana Mussa, Lucy Mpayo, Benson Mboya, Comfort Peter, Ilenedy Bongezi, Edwin Mwimbula, Emmanuel Messy, Azizi Mohammed na Anna Tarimo.

Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo, huku wakili wao wakiiomba mahakama hiyo kutoa Sh milioni 40 ya fedha hizo ili ziweze kugawanywa kwa washtakiwa wote waweze kupewa dhamana.

Hata hivyo, Hakimu Mmbando aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 11, mwaka huu kwa ajili ya kutoa uamuzi na washtakiwa hao wamerudishwa rumande.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles