23.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Watalaamu zao la mpunga Afrika wakutana kuchangamoto za zao hilo

Na Esther Mnyika Mtanzania Digital

Wataalamu na Wadau wa Uzalishaji Mpunga (RBI) wa nchi za Afrika Mashariki na Kusini wamekutana kujadili changamoto mbalimbali na kutoa tathimini za utafiti wa kuendeleza la zao mpunga katika nchi hizo.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) , Dk.Geoffrey Mkumilo.

Hayo yamebainishwa Agosti 28 jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa siku tatu wa wadau wa zao la hilo uliojumuisha nchi 11 na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli amesema washiriki wa uzalishaji mpunga wataleta mkakati wa kuboresha uzalishaji wa zao hilo kwa nchi za Afrika Mashariki na Kusini.

Amesema Tanzania kuwa na nguvu kubwa katika kuendeleza mpunga kama mazao muhimu ushirikiano wa wakulima, taasisi za utafiti haswa TARI na mashirika ya kimataifa.

“Tanzania kwenye takwimu zinaonyesha inashika nafasi ya pili Afrika kwa kuzalisha zao la Mpunga ikiwa inaongoza Madagascar hivyo Taasisi ya Utafiti wa Mpunga Kimataifa (IRRI) imeona Tanzania ina eneo lina maji na ardhi ya kuzalisha mpunga zaidi,”amesema Mweli.

Amesema zao la mpunga ni chakula na ni biashara soko la ndani ni kubwa na nje ya nchi ni kubwa uzalishaji bado mdogo.

“Serikali ina pigania mabadiliko katika matumizi ya mpunga ya teknolojia ya kilimo ili kuongeza uzalishaji wa mpunga. Kutoka chini ya tani 2.5 kwa hekta hadi tani tano au zaidi ifikapo mwaka 2030,” amesema.

Amesema lengo la serikali kuzalisha mpunga wa kutosha kukidhi mahitaji ya kitaifa kuchangia katika kula na usalama wa chakula kote Afrika na kuwa mzalishaji namba moja wa mpunga Barani. Aidha amesema kwa programu ya RBI ni ushirikiano wa sekta muhimu na binafsi uliolenga kula na kutumia aina bora za mpunga kwa wakulima wadogo katika Afrika Mashariki na Kusini. Mweli anasema Tanzania ina jukumu kubwa kama mzalishaji wa mpunga na mipango inatekelezwa na IRRI.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Dk. Geoffrey Mkumilo amesema katika mkutano huo wanatarajia mikakati mikubwa na nchi yetu ardhi yake ya kuzalisha Kilimo cha umwagiliaji na mvua.

“Tanzania ni moja wapo ya wazalishaji wakuu wa mpunga Afrika lakini bado kuna nafasi kubwa ya kuboresha kiwango chetu cha wastani wa tani 2.5 kwa hekta ni eneo ambalo linahitaji umakini wa kitaifa, kikanda na kibara,”amesema Dk. Mkumilo.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Kikanda wa IRRI Afrika, Dk. Abdelbagi Ismail amesema Tanzania na nchi nyingi za Afrika Mashariki na Kusini kuchochea maboresho katika uzalishaji wa mpunga ili kupambana na njaa, umaskini wa kipato kwa mamilioni ya wakulima wadogo. Amesema mpunga ni chakula, biashara na ni uhai kwa mamilioni watu na wana jukumu la pamoja la kubuni na kuongeza uzalishaji wake kwa njia endelevu.

“Naamini kwa pamoja tunaweza kutimiza mengi zaidi na kuleta tofauti ambayo hakuna mmoja wetu angeweza kufanya pekee yake tuendelee na ushirikiano huu mzuri ,”amesema Dk. Ismail.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles