30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

WATAKAOHUJUMU MIUNDOMBINU TANESCO KUKIONA

Hadija Omary, Lindi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuilinda na kuitunza miundombinu ya Shirika la Umeme nchini (Tanesco), huku akiagiza mamlaka husika kuwashughulikia watakaojihusisha na uharibifu wa miundombinu hiyo.

Majaliwa ameyasema hayo leo Mei 21, alipokuwa akizindua uunganishaji wa gridi ya taifa kwa Mkoa wa Lindi na Mtwara iliyofanyika katika Kituo cha kupozea umeme cha Maumbika mkoani hapa.

“Wapo baadhi ya watu wasio na nia njema na serikali wanaharibu miundombinu kwa kung’oa vyuma na kuuza kama vyuma chakavu, hawa ni wahujumu uchumi.

“Naagiza mamlaka zinazohusika kufanya ukaguzi kila eneo linalouza au kununua chuma chakavu kubaini kama kuna miundombinu ya Tanesco na endapo mtaikuta wahusika wawajibishwe kwa mujibu wa sheria,” alisema Majaliwa.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Majaliwa amesema kuwa mkakati uliopo sasa ni kuboresha miundombinu ya zamani na kujenga miradi mipya ya umeme ili kuzalisha umeme wa kutosha ili kuwafikia wananchi wengi.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles