26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 5, 2023

Contact us: [email protected]

Watahiniwa 485,866 kuanza mitihani kitato cha nne leo

Faraja Masinde -Dar es salaam

WATAHINIWA 485,866,  leo wanaanza mtihani wa kuhitimu kidato cha nne mwaka 2019.

Kati ya watainiwa hao, 433,052 ni wa shule  na 52,814 wakujitegemea.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la  Mitihani(Necta), Dk. Charles Msonde alisema kuongezeka kwa watahiniwa kumetokana na kazi nzuri inayofanywa na Serikali, ikiwamo kuwaibua wanafunzi wenye mahitaji maalumu kwa sababu ni mpango wa kuhakikisha kila mmoja anapata elimu.

“Mtihani wa kidato cha nne (CSEE) na Maarifa(QT), utafanyika kuanzia kesho (leo) Novemba 4 hadi 22,shule za sekondari 4,933 na vituo vya watahiniwa wa kujitegemea 1,050.

“Kati ya watainiwa wa shule 433,052 waliosajiliwa, wanaume ni 206, 420 sawa na asilimia 47,67 na wanawake ni 226,632 sawa na asilimia 52.33. Watahiniwa wenye mahitaji maalumu wapo 842 kati yao 450 ni wenye uoni gafifu, 42 ni wasioona, 200 ni wenye ulemavu wa kusikia na 150 ni wenye ulemavu wa viungo vya mwili,” alisema Dk. Msonde.

Alisema mwaka jana , idadi ya wataini wa shule waliosajiliwa walikuwa 427,181, hivyo kuna ongezeko la watainiwa  5,871 sawa na asilimia 1.37 mwaka huu,ikilinganishwa na mwaka jana.

“Kati ya watainiwa wakujitegemea 52,814 waliojisajili, wanaume ni 23,418 sawa na asilimia 44,34 na wanawake ni 29,396 sawa na asilimia 55.66. Watahiniwa wa kujitegemea wenye mahitaji maalumu wako 28 ambapo wenye uoni hafifu ni 20 na wasioona ni 8, ambapo mwaka jana idadi ya wataini wa kujitegemea waliosajiliwa ilikuwa ni 58,954.

“Mtihani wa Maarifa (QT),watahiniwa wa 12,984 wamesajiliwa kufanya mtihani huoambapo wanaume ni 5,493 sawa na asilimia 42,30 na wanawake ni 7,491 sawa na asilimia 57.70, ikilinganishwa na mwaka jana ambapo idadi ilikuwa 14,348,” alisema Dk. Msonde.

Kuhusu umuhimu na maandalizi ya mtihani huo, alisema maandalizi yote yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambaza kwa mtihani, vitabu vya kujibia na nyaraka zote muhimu zinazohusu mtihani huo katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.

“Mtihani wa kidato cha nne ni muhimu kwa wananfunzi na jamii kwa ujumla kwa kuwa hupima uwezo na uelewa wa wanafunzi katika yale yote waliyojifunza  kwa kipindi cha miaka mine.

“Ikumbukwe  matokeo ya mtihani huu hutumika kuchaguzi  wanafunzi wanaojiunga na elimu ya juu na sekondari (kidato cha tano) pamoja na fani mbalimbali za utaalamuwa kazi kama vile afya, kilimo, ualimu, ufundi na nyingine, ni mtihani muhimu kwa wanafunzi, wazazi, jamii nzima na taifa kwa ujumla,” alisema .

Katika hatua nyingine, Dk. Msonde, alitumia nafasi hiyo kutoa wito kwa kamati za mitihani za mikoa na halmashauri kuhakikisha  taratibu zote za uendeshaji wa mitihani ya taifa zinazingatiwa ipasavyo.

“Kamati zihakikishe  mazingira ya vituo vya mitihani yapo salama, tulivu na kuzuia mianya yote inayoweza kusababisha kutokea kwa udanganyifu. Kamati zote zinaelekezwa pia kuhakikisha usalama wa vituo teule unaimarishwa na  vituo vitumike kwa kuzingatia mwongozo uliotolewa na baraza,” alisema.

Aliwataka wasimamizi wote walioteuliwa kufanya kazi yao ya usimamizi kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu, ikiwa ni pamoja na kuzingatia kanuni na miongozo waliyopewa.

“Wasimamizi wahakikishe kuwa wanalinda haki ya watainiwa wenye mahitaji maalum, ikiwa ni kuwapa mitihani yenye maandishi yaliyokuzwa kwa watahiniwa wenye uono hafifu, kuongeza muda kwa watainiwa wote wenye mahitaji maalumu wa dakika 20 kwa kila somo la hisabati na dakika 10 kwa kila saa kwa masomo mengine.

“Wanafunzi pia baraza linaamini  walimu wamewaandaa vizuri  kipindi chote cha miaka minne ya elimu ya sekondari,ni matarajio yetu  watafanya mitihani yao kwa kuzingatia kanuni za mitihani ili matokeo yaoneshe uwezo halisi kulingana na maarifa ya ujuzi waliopata,” alisema

Wamiliki wa shule waonywa

Katika hatua nyingine, Dk. Msonde, aliwaonya wamiliki wa shule kwa kuwataka watambue  shule zao ni vituo maalumu vya mitihani,hawatakiwi kwa namna yoyote kuingilia majukumu ya wasiamamizi wa mitihani katika kipindi chote cha ufanyaji wa mtihani huo.

“Baraza halitosita kukifuta kituo chochote cha mitihani endapo litajiridhisha pasipo shaka  uwopo wake unahatarisha usalama wa mitihani ya taifa. Pia baraza linawaasa wasiamamizi wa mitihani, wamiliki wa shule, walimu na wananchi wote kwa ujumla kutokujihusisha na vitendo vyovyote vya udanganyifu.

“Baraza halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kujihusisaha au kusababsiha udanganyifu wa mitihani kwa mujibu wa sheria za nchi yetun a kanuni za utumishi wa umma, wadau wote wanaombwa kutoa taarifa katika vyombo husika kila wanapobaini uwapo wa mtu au kikundi cha watu kujihusisaha na udanganyifu wa mitihani wa aina yoyote ile,” alisema Dk. Msonde.

Udanganyifu wapungua

Katika hatua nyingine, Dk. Msonde, alisema vitendo vya udanganyifu vimeendelea kupungua kila mwaka ikilinganishwa na miaka ya nyuma jambo ambalo limevutia nchi nyingine kuja kujifunza.

“Udanganyifu kwenye matokeo ya mitihani umekuwa ukipungua mwaka hadi mwaka, mfano mwaka 2011 watahiniwa wa shule za msingi 9,736 tuliwafutia matokeo kwa udanganyifu ikilinganishwa na mwaka jana ambao walikuwa 230, huku sekondari waliofanya udanganyifu 2011, walikuwa 3303,mwaka jana walikuwa 200.

“Juhudi hizi zinatokana na kazi kubwa inayofanywa na kamati zetu mbalimbali pamoja na Serikali kwa ujumla, jambo hili limefanya hadi mwaka jana tumepokea nchi 10 amabzo zilikuja kujifunza kwetu namna ambavyo tumeweza kudhibiti udanganyifu, hivyo ni wajibu wa kila mmoja kufanya kwa nafasi yake, nchi hii ni kubwa,” alisema Dk. Msonde.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles