27.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

Wataalam wakuna vichwa kudhibiti Malaria nchini

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digita

Wakati Tanzania ikipambana kuhakikisha inatokomeza Malaria wataalamu wameeleza kuwa moja ya changamoto inayokwamisha juhudi hizo ni pamoja na matokeo ya tafiti mbalimbali zinazofanyika kushindwa kuwafikia walengwa.

Hayo yamebainishwa leo Mei 30, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Afya ya Uzazi Mama na Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Dk. Ahmad Makuwani katika mkutano uliowakutanisha watafiti na wadau mbalimbali wa sekta ya afya ukiwa na lengo la kujadili jinsi ya kutomeza malaria nchini ifikapo mwaka 2030.

“Tfiti nyingi zimekuwa zikifanyika zikiwamo zinazohusu malaria, lakini jambo tulilobaini nikwamba tafiti hizi zimekuwa haziwafikii walengwa, hivyo unakuta kwamba wanashindwa namna ya kutumia tafiti hizi.

“Kwani kila mmoja wetu hapa ni shahidi kwamba tunahitaji kutokomeza ugonjwa huu ifikapo mwaka 2030,” amesema Dk. Makuwani ambaye alimwakilisha Mganga Mkuu wa Serikali.

Amesema watafiti hao wanajiuliza maswali kwa nini mikoa kama Arusha, Manyara, Kilimanjaro na mingine imefikisha asilimia moja kupunguza malaria na kwa nini imekuwa changamoto kwa mikoa mingine ambayo bado ina viwango vya juu vya ugonjwa huo hatari.

Aidha, amefafanua kuwa hali ya ungonjwa wa malaria siyo nzuri kuna mikoa bado ipo kwenye asilimia 15 hadi 20 ambayo ni Kanda ya Ziwa na Pwani na bado ugonjwa huo unaua watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

“Wenzetu Zanzibar wamefanikiwa kutomeza malaria bado bara, watafiti wanaumiza kichwa kwenye mkutano huu kutafuta majibu yatakayo tusaidia kupata mwarobaini na uwezo wa kutokomeza ugonjwa wa malaria ifakapo mwaka 2030,” amesisitiza Dk. Makuwani.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Afya Ifikara, Dk. Honorati Masanja amesema sababu zinazosababisha ongezeko la maralia nchini ni tabia za watu kutokuhudhuria hospitali kwa wakati pindi wanapopata malaria.

Amesema badala yake wanajitibu kienyeji hali inayosababisha vijidudu vya malaria kuongezeka na kusababisha madhara makubwa kwa mgonjwa wakati mwingine kupelekea kifo.

“Kuna sababu nyingi zinazosababisha ongezeko la malaria kwa baadhi ya mikoa ikiwa ni pamoja na tabia za watu na hizi afua za maralia kutowafikia walengwa kwa wakati,”amesema Dk. Masanja.

Naye Mwakilishi kutoka Zanzibar, Safia Mohamed Ali amesema Zanzibar imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokomeza ugonjwa huo sababu ya udogo wa kisiwa hicho na kutoa elimu jumuishi ya kupambana na ugonjwa huo.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Bunge kwenye mkutano huo, Dk. Hamis Kigwangalla amesema Bunge kwa nafasi yao wataishauri Serikali kutumia mbinu ambazo zitasaidia kutokomeza maralia kwani lengo kufikia zero malaria ifikapo 2030

Aidha, Kigwangala ameongeza kuwa Zanzibar imefanikiwa kutokomeza malaria kwani wao walijikita moja kwa moja kwenye kutokomeza wakati bara walijitika kwenye kudhibiti hali iliyosababisha mafanikio makubwa wa Zanzibar.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles