31 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wataalam Bondela Wami/Ruvu wafanya ukaguzi wa vyanzo vya maji

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Timu ya Wataalam kutoka Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imeendelea kufanya ukaguzi wa matumizi ya maji kutoka maeneo mbalimbali ya vyanzo vya maji.

Wataalamu hao walipo katika zone ya Mto Lukulunge na Ngerenge imefanikiwa kubaini mifereji zaidi ya mitatu na kuifunga yote kwa pamoja upande wa juu wa Mto Lukulunge ambayo ilikuwa imebadilisha uelekeo na kupunguza wingi wa maji mtoni.

Aidha, timu hiyo ya wataalam imebaini uvunaji wa maji kwa kutumia Pump unaofanywa na askari kikosi cha jeshi la Wananchi. Pump hiyo imekabidhiwa kwa Mkuu wa kikosi cha Mbinga na kupewa elimu ya usimamizi wa Rasilimali za maji ili iwe mfano kwa sehemu ya watumiaji wa Maji.

“Baadda ya ukaguzi huu tuliofanya kutoka zone ya Ruvu Chini timu ya wataalam wa bonde la Wami/Ruvu imefanikiwa kubaini uchepushwaji wa Maji kutoka Mto Ruvu unaofanywa na mwekezaji wa mabwawa ya samaki anayefahamika kwa jina la Eliona Koka wa kijiji cha Kisabi kata ya Muungano Halmashauri ya Kibaha mkoani Pwani.

“Katika ukaguzi huo timu ya wataalam wa Bonde la Wami wakiambatana na Wataalam wa Mamlaka ya Maji Dawasa wamefanikiwa kubaini matumizi ya maji isivyo halali kinyume na Sheria ya rasilimali za Maji ya Mwaka 2009,” imeeleza taarifa ya wataalamu hao.

Aidha, mmiliki huyo amekutwa akiendesha shughuli za ufugaji wa samaki katika vizimba huku akiwa hana vibali vya matumizi ya maji kutoka mtoni jambo linalopelekea kuvunja sheria ya usimamizi wa rasilimali za maji.

Wakizungumzia ukaguzi huo wataalamu hao wamesema kuwa ulilenga kufanya tathimini ya maji pamoja na kutoa elimu ya urasimishaji wa matumizi na utunzaji wa rasilimali za maji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles